Waslavi (kwa Kiingereza Slavs, pia "Slavic" au "Slavonic people") ni kundi kubwa la mataifa yanayotumia lugha za Kihindi-Kiulaya barani Ulaya. Pamoja na kuwa wenyeji wa nchi za Ulaya Mashariki, Ulaya ya Kati na Ulaya Kusini kuanzia karne ya 6 BK, tangu zamani wameenea Asia Kaskazini na Asia ya Kati. Nchi zao zinatawala zaidi ya 50% za bara la Ulaya.

Lugha za Kislavi Ulaya.
Ramani ya dunia ikionyesha wapi Waslavi ni      wengi kuliko makabila mengine     zaidi ya 10% za wakazi wote

Tofauti hariri

Wanagawanyika kati ya Waslavi wa Magharibi (hasa Wapolandi, Wacheki na Waslovaki), Waslavi wa Mashariki (hasa Warusi, Wabelarus na Waukraina), na Waslavi wa Kusini (hasa Waserbi, Wakroati, Wabosnia, Wamakedonia, Wasloveni, Wamontenegro na Wabulgaria).

Mahusiano yao yanatofuatiana, kuanzia hisia ya kuwa na mengi ya pamoja hadi kuchukiana kabisa na kupigana vita kwa ukatili.[1]

Idadi hariri

Duniani kote Waslavi wanakadiriwa kuwa milioni 360. Kati yao wanaongoza Warusi, Wapolandi na Waukraina.

Tanbihi hariri

  1. Robert Bideleux; Ian Jeffries (January 1998). A History of Eastern Europe: Crisis and Change. Psychology Press. ISBN 978-0-415-16112-1. 
  Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Waslavi kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.