Ukraine

(Elekezwa kutoka Waukraina)

Ukraine (kwa Kiukraine: Україна, Ukrayina) ni nchi ya Ulaya ya Mashariki. Imepakana na Urusi, Belarus, Poland, Slovakia, Hungaria, Romania na Moldova.

Україна
Ukrayina

Ukraine
Bendera ya Ukraine Nembo ya Ukraine
Bendera Nembo
Kaulimbiu ya taifa: --
Wimbo wa taifa: Ще не вмерла України
Shche ne vmerla Ukrajiny]]
"Ukraine's glory has not perished"
Lokeshen ya Ukraine
Mji mkuu Kiev (Kyiv)
50°27′ N 30°30′ E
Mji mkubwa nchini Kiev
Lugha rasmi Kiukraine
Serikali Demokrasia
Petro Poroshenko
Volodymyr Hroysman
Uhuru
ilitangazwa
Kura ya maoni ya wananchi
ilikubaliwa
24 Agosti 1991
1 Desemba 1991
25 Desemba 1991
Eneo
 - Jumla
 - Maji (%)
 
603,700 km² (ya 44)
7%
Idadi ya watu
 - 2014 kadirio
 - 2001 sensa
 - Msongamano wa watu
 
44,291,413 (ya 32)
48,457,102
73.8/km² (ya 115)
Fedha Hryvnia ya Ukraine (UAH)
Saa za eneo
 - Kiangazi (DST)
EET (UTC+2)
EEST (UTC+3)
Intaneti TLD .ua
Kodi ya simu +380

-


Ramani ya Ukraine leo.

Kuna pwani ya Bahari Nyeusi na ghuba ya Azov.

Mji mkuu ni Kiev (Kyiv).

HistoriaEdit

Historia ya kaleEdit

 
Dola la Kiev, chanzo cha Urusi.

Ukraine ulianza polepole pamoja na Urusi huko makabila ya wasemaji wa Kislavoni cha Mashariki walikoanza kujenga maeneo yao kuanzia karne ya 8 BK.

Waviking waliunda dola la kwanza katika eneo la Kiev, wakalitawala kama dola la Kislavoni. Wenyewe waliingia haraka katika lugha na utamaduni wa wenyeji, lakini waliacha jina lao kwa sababu "Rus" kiasili ilikuwa jina la Waskandinavia wale kutoka Uswidi ya leo.

Mwaka 988 Kiev ilipokea Ukristo wa Kiorthodoksi kutoka Bizanti. Tukio hilo liliathiri moja kwa moja utamaduni na historia yote iliyofuata.

Dola la Kiev liliporomoka kutokana na mashambulio ya Wamongolia baada ya Jingis Khan, na maeneo madogo zaidi yalijitokeza yaliyopaswa kukubali ubwana wa Wamongolia.

Upanuzi wa utemi wa MoscowEdit

Kubwa kati ya maeneo yale madogo ulikuwa utemi wa Moscow. Watemi wa Moscow walichukua nafasi ya kwanza kuunganisha Waslavoni wa Mashariki dhidi ya Wamongolia na kupanua utawala wao.

Hivyo kwa muda mrefu Ukraine ilikuwa sehemu ya Dola la Urusi.

Miaka mia ya mwishoEdit

Miaka 1918 - 1921 baada ya mwisho wa Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia na ya kuporomoka kwa Dola la Urusi nchi ilikuwa na kipindi kifupi cha uhuru na vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Miaka 1922 - 1991 Ukraine ilikuwa jamhuri mwanachama wa Umoja wa Kisovyeti.

Hatimaye ilijipatia tena uhuru wake, ingawa Russia haijaridhika wala kukubali mipaka. Hivyo mwaka 2014 ilivamia rasi ya Krimea na maeneo mengine ya mashariki. Hadi leo hali ni ya vita.

WakaziEdit

Sensa ya mwaka 2001 ilionyesha ya kwamba 77.8% za wakazi hujiita "Waukraine". Waliojiita Warusi walikuwa 17.3%. Vikundi vingi vingine kama Wabelarus, Wamoldova, Watartari, Wabulgaria, Wapoland, Wayahudi na wengine walikuwa kila kimoja chini ya 1%.

LughaEdit

Kwa muda mrefu Ukraine ilitawaliwa na Urusi na Kirusi kilikuwa lugha ya utawala hali halisi. Hivyo wengi wamezoea Kirusi, hata kati ya Waukraine asilia; hivyo Kiukraine kilikuwa lugha mama ya % 67.5, Kirusi ya % 29.6.

Tangu uhuru serikali imeendesha sera ya kujenga lugha ya taifa, pamoja na kujali lugha nyingine 18 za kieneo.

Hivyo lugha rasmi ni Kiukraine (українська мова "ukrajin's'ka mova"), mojawapo kati ya lugha za Kislavoni, karibu sana na Kirusi, lakini angalau nusu ya wakazi hutumia pia Kirusi.

DiniEdit

Baada ya ukomunisti kupiga vita dini kwa njia zote na kwa miaka mingi, siku hizi wakazi wengi wamerudia dini zao.

Walionayo ni hasa Wakristo (81.9%), wakiwemo wale wa Kanisa la Kiorthodoksi la Russia (23%), lakini Waorthodoksi wengine wamejitenga na kuanzisha Kanisa la Kiorthodoksi la Ukraina (40.8%).

Pia kuwa waamini wengiwengi wa Kanisa Katoliki (10.2%), hasa wa Kanisa Katoliki la Kigiriki la Ukraina (9.4%) linalofuata mapokeo ya Kigiriki kama Waorthodoksi, lakini pia wa Kanisa la Kilatini (0.8%).

Waprotestanti ni 2.2% na Waislamu 1.1%.

Pamoja na hayo, idadi ya wakazi inazidi kupungua haraka (-12.8% kati ya 1993 na 2014).

Tazama piaEdit

Viungo vya njeEdit

  Makala hii kuhusu maeneo ya Ulaya bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Ukraine kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.