Lugha za Kihindi-Kiulaya

Lugha za Kihindi-Kiulaya ni jamii ya lugha iliyo kubwa kuliko zote duniani. Imekadiriwa kuna lugha hai 445 za jamii hiyo na wasemaji bilioni 3.2 katika mabara yote (46% za watu wote wa leo).

Uenezi wa lugha za Kihindi-Kiulaya (kijani cheupe) kati ya jamii za lugha nyingine duniani.
Uenezi wa wasemaji wa Kihindi-Kiulaya asilia kufuatana na nadharia ya Kurgan
Uenezi katikati ya milenia ya 3 KK
Uenezi katikati ya milenia ya 2 KK
Uenezi takriban mwaka 250 KK

Uenezi huo umetokana hasa na historia ya ukoloni wa Kizungu uliopeleka lugha za Ulaya pande zote za dunia.

Lugha zenye wasemaji zaidi ya milioni 100 ni: Kihispania, Kiingereza, Kihindustani (Kihindi/Kiurdu), Kireno, Kibengali, Kipanjabi na Kirusi.

Nyingine zenye wasemaji zaidi ya milioni 50 ni: Kijerumani, Kifaransa, Kimarathi, Kiitalia na Kiajemi.

Lugha za Kihindi-Kiulaya

Jina la Kihindi-Kiulaya hariri

Jina la Kihindi-Kiulaya limepatikana tangu karne ya 19. Wataalamu walitambua ya kwamba lugha za kale zinazotunzwa kimaandishi kama Kilatini, Kigiriki, Kisanskrit na Kiajemi cha Kale zinafanana kati yake pia na lugha nyingine za kisasa za Ulaya na Uhindi wa Kaskazini.

Lugha za jamii ya Kihindi-Kiulaya zinafanana katika msamiati na sarufi.

 
     Lugha rasmi kuu     Lugha rasmi ya pili     Iliyotambulika kisheria     Ya maana     Haitumiki

Nadharia ya asili na usambazaji hariri

Inaaminika ya kwamba lugha hizo zilikuwa na asili moja katika lugha isiyojulikana tena ya Kihindi-Kiulaya asilia.

Wasemaji wake wanaaminiwa kuwa walisambaa takriban miaka 6,000 iliyopita kutoka sehemu za Asia ya Magharibi. Sehemu ilikwenda magharibi na kuingia Ulaya, sehemu nyingine ilikwenda Uajemi na Bara Hindi.

Kuna nadharia mbalimbali kuhusu historia hiyo.

Kati ya lugha hizo kuna zifuatazo:

( † inamaanisha ya kwamba lugha hii haina wasemaji tena kama lugha hai)

Marejeo hariri

     . https://openaccess.leidenuniv.nl/bitstream/handle/1887/2660/299_011.pdf.

Marejeo mengine hariri

Viungo vingine hariri

 
Wikimedia Commons ina media kuhusu:

Databases hariri

Lexica hariri

  Makala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Lugha za Kihindi-Kiulaya kama historia yake, uenezi au maendeleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.