Wayne Palmer
Wayne Palmer ni jina la uhusika wa kipindi cha televisheni cha Kimarekani maarufu kama 24. Uhusika ulichezwa na D. B. Woodside.
Wayne Palmer | |
---|---|
muhusika wa 24 | |
D. B. Woodside kama Wayne Palmer | |
Imechezwa na | D. B. Woodside |
Misimu | 3, 5, 6 |
Maelezo |
Katika uhusika
haririHuyu ni ndugu wa Rais wa zamani wa Marekani Bw. David Palmer, Wayne alikuja kuchukua nafasi ya Mike Novick na alifanya kazi kama Mkubwa wa Wafanyakazi wa Ikulu, ni baada ya Palmer kumhondosha Novick kazini mwishoni mwa Msimu wa Pili.
Zamani alifanya kazi kama askari wa Majini wa Marekani. Pia, ana dada yake aitwaye Sandra Palmer. Baada ya kumaliza elimu ya juu, akapata ufadhili wa baseball katika Chuo Kikuu cha Stanford, ambapo alipata digrii ya Sayansi ya Siasa.
Baadaye, alienda kupata digrii ya Sheria, ambayo ameipata katika Chuo cha Sheria cha Yale. Inaaminika ya kwamba, huyu naye ni kama kaka yake, Wayne Palmer naye ni mwanachama wa chama cha Democrat.
Viungo vya Nje
hariri- Character biography Ilihifadhiwa 25 Februari 2007 kwenye Wayback Machine. on the official 24 website