Wikipedia:Makala ya wiki/Hastings Banda
Hastings Kamuzu Banda (1898 - 25 Novemba, 1997) alikuwa daktari na mwanasiasa aliyeendelea kuwa kiongozi, rais na dikteta wa Malawi tangu mwaka 1961 hadi 1994. Kamuzu Banda alizaliwa karibu na Kasungu, Malawi iliyokuwa wakati ule sehemu ya eneo lindwa la Afrika ya Kati ya Kiingereza (baadaye Nyasaland). Wazazi walikuwa Mphonongo Banda na Akupingamnyama Phiri. Tarehe ya kuzaliwa haijulikani ilhali wakati ule hakukuwa na utaratibu wa kuandikisha watu. Alikubali baadaye matokeo ya utafiti wa rafiki kutoka Marekani aliyekadiria ya kwamba alizaliwa mnamo Machi au Aprili 1898 Jina lake Kamuzu lamaanisha "mzizi mdogo" kwa sababu alizaliwa baada ya mama yake kutumia dawa ya mitishamba kwa kusudi la kupata mimba Mnamo 1915–1916 Banda aliondoka kwao akisafiri Afrika Kusini ... Mwaka 1925 Banda aliondoka kwenda Marekani. 1958 alirudi Nyasaland. Kwenye mkutano wa Nyasaland African Congress (NAC) alichaguliwa mara moja kuwa kiongozi. Alizunguka nchini akiwahutubia watu na kudai uhuru wa Unyasa. Mwaka 1964 aliongoza nchi kwenye uhuru kamili. Banda aliamua kubadilisha jina kutoka Nyasaland kuwa "Malawi". ►Soma zaidi