Wikipedia:Mwongozo (Muundo)

(Elekezwa kutoka Wikipedia:Ukufunzi (Muundo))
Utangulizi   Kuhariri   Kuanzisha Makala   Muundo   Viungo vya Wikipedia   Kutaja vyanzo   Kurasa za majadiliano   Kumbuka   Kujisajili    

Kupanga umbo la maandishi ni tofauti kidogo na kuandika kwenye kichakata matini (programu ya kuandika) kama vile Word, Writer na kadhalika.

Dirisha la hariri na WYSIWYG

Unaandika katika dirisha la uhariri. Humo huoni umbo la maandishi jinsi inavyotokea baadaye. Maana hapa hakuna kile kinachoitwa "WYSIWYG" ("What You See Is What You Get unachoona ni sawa kile kinachotokea").

Badala yake Wikipedia hutumia misimbo (codes) inayosababisha kutokea kwa maandishi manene, makubwa, madogo, ya rangi, vichwa au viungo na kadhalika. Hii ni lugha ya kompyuta ya pekee inayoitwa wikitext ikifanana na HTML lakini imerahisishwa.

Herufi koza na italiki

Misimbo inayotumika hasa kwenye Wikipedia ni Herufi koza' na italiki. Yote mawili hupatikana kwa kuingiza neno / maneno kwa alama za apostrofi ('').

Unaandika Unapata
''italiki'' italiki

'''koza'''

koza

'''''koza italiki'''''

koza italiki

Kwa kawaida si lazima kutaipu apostrofi moja-moja. Unaweza kuangaza neno au maneno husika kwa puku yako na kutumia menyu (nembo dogo) juu ya dirisha la uhariri. "B" inakupa herufi koza, "I" inaleta herufi italiki.

Jina la makala ya Wikipedia inatakiwa kuonekana kwa herufi koza pale inapoonekana mara ya kwanza ndani ya makala, mara nyingi kama neno / maneno ya kwanza. Vinginevyo hatutumii herufi koza, isipokuwa ikisaidia kupanga matini marefu yasomeke vizuri zaidi pale ambako hatutaki kutumia vichwa vya habari.

Mfano: Makala ya Julius Nyerere inaanza:

"Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alikuwa rais wa kwanza wa Tanzania. Alizaliwa Butiama, mkoani Mara pembezoni mwa Ziwa Nyanza tarehe 13 Aprili, 1922..."

Herufi italiki hutumiwa kwa ajili ya majina ya vitabu, filamu au albamu za muziki. Pia kwa kuonyesha matamshi ya neno la kigeni.


Vichwa na vichwa vidogo

Vichwa na vichwa vidogo vya ndani ni njia ya haraka kuboresha mpangilio wa makala. Kama maandishi ni marefu kiasi ni afadhali kuingiza vichwa hivi. Ni muhimu kuwa na muundo 1 kwa makala zote maana hii inawasaidia wasomaji wasipate kuzoea uso mbalimbali ndani ya makala zetu.

Tahadhari 1: Usiweke kichwa juu ya makala yako (yaani mwanzoni wa maandishi yote) kwa sababu wikipedia inafanya hii pia!
Tahadhari 2: Usiweke vichwa nje ya utaratibu huu: usitumie mstari yenye HERUFI KUBWA au mstari mwenye maandishi koza kama vichwa vya ndani.

Vichwa huanzishwa kwa njia hiyo (hakuna alama kwa kazi hii kwenye menyu)

Unaandika Unapata

== Kichwa ==

Kichwa

=== Kichwa kidogo 1 ===

Kichwa kidogo 1

==== Kichwa kidogo 2 ====

Kichwa kidogo 2

Kama vichwa 4 au zaidi vimeshaingizwa katika makala sanduku ya yaliyomo inaanzishwa na programu peke yake. Tazama juu: sanduku hili limejitokeza tu bila kazi ya ziada kwa sababu kuna vichwa vinne kwenye ukurasa!

Makosa ya kawaida

Makosa hutokea na wewe hutakuwa mtu wa kwanza kwenye wikipedia kufanya makosa. Lakini sisi sote tunapenda kuboresha wikipedia na uwezo wetu wa kuchangia. Ili ujifunze juu ya makosa yanayotokea mara kwa mara angalia Wikipedia:Makosa!

Jaribu kuandika kichwa kwenye sanduku la mchanga wa ukurasa huu.

Jaribu ulichojifunza katika sanduku la mchanga


Endelea mwongozo na Viungo vya Wikipedia