Wilaya ya Newala Vijijini
Wilaya ya Newala ni moja ya wilaya za Mkoa wa Mtwara. Katika sensa ya mwaka 2012, idadi ya wakazi wa wilaya hiyo ilihesabiwa kuwa 205,492.
Wilaya hii imepakana na Wilaya ya Masasi upande wa magharibi na kaskazini, wilaya ya Tandahimba upande wa mashariki na kaskazini, mto Ruvuma na Msumbiji kwa kusini. Newala imepakana kwa karibu kabisa na nchi ya Msumbiji ambapo mto Ruvuma ndio unaotenganisha wilaya ya Newala na nchi ya Msumbiji.
Wakazi walio wengi ni Wamakonde, pamoja na Wayao.
Idadi kubwa ya wakazi wa wilaya ya Newala ni wakulima na zao kuu la biashara ni korosho.
Mnamo mwaka 2015 maeneo ya Newala mjini yalipewa halmashauri ya pekee na hivyo kutengwa na Wilaya ya awali[1].
Marejeo
haririViungo vya Nje
haririMakala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Mtwara bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Wilaya ya Newala Vijijini kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno. |
Kata za Wilaya ya Newala Vijijini - Tanzania | ||
---|---|---|
Chihangu | Chilangala | Chitekete | Chiwonga | Kitangari | Makukwe | Malatu | Maputi | Mchemo | Mdimba Mpelepele | Mikumbi | Mkoma II | Mkwedu | Mnyambe | Mnyeu | Mpwapwa | Mtopwa | Mtunguru | Muungano | Nakahako | Nambali | Nandwahi |