Korosho ni mbegu wa mkorosho[1] ni mmea wa jamii ya mimea itoayo maua ya familia ya Anacardiaceae.

Korosho
Mabibo mtini ilhali korosho zipo chini ya tunda

Korosho yenyewe inakua pamoja na tunda linaloitwa bibo ilhali mbegu unaonekana nje ya bibo.

Mmea huu ni wa asili ya kaskazini mashariki mwa Brazili, lakini sasa hukua sana maeneo ya tropiki, kwa ajili ya mbegu yake ya korosho na bibo zake.

Jina lake la Kiingereza limetokana na neno la Kireno ambalo lina asili ya Tupi.

Makazi na makuzi

hariri

[1] occidentale tree.jpg Ni mmea mdogo ambao huwa wa kijani nyakati zote,kufikia urefu wa mita 10 – 12; na shina fupi lisilo na umbo maalum. Majani yamejipanga kwa mzunguko yenye asili ya ngozi na urefu wa sm 22 na upana wa sm 2 -15. Maua laini huzalishwa yakiwa na urefu wa sm 26, na huanza na rangi nyepesi ya kijani mwanzoni lakini baadae hugeuka na kuwa jekundu na petali zenye urefu takribani mm 7 mpaka 15.

Kitu ambacho huonekana kama tunda ambacho hukua katika kikonyo cha ua la mmea wa korosho; tunda hilo huitwa bibo, na huiva na kuwa la njano, huku likiwa na ukubwa was m 5 mpaka 11. Bibo huliwa na ladha tamu na harufu nzuri. Ndani mwake kuna majimaji ya kutosha lakini ngozi yake ni laini mno hivyo kufanya usafirishaji kuwa mgumu kwelikweli.

Tunda la ukweli la mkorosho ni korosho yenyewe lenye umbo la figo au ghofu ya mabondia ambalo hukua juu ya tunda la bibo ndani ya tunda hili la kweli ndio kuna mbegu moja, korosho. Mbegu imezungukwa na makombe/ ngozi mbili ndani ya ngozi mbili huwa na kemikali inayofahamika sana inayosababisha mwasho kwa baadhi ya watu lakini mafuta ya korosho huwa na athari ndogo ukilinganisha na mafuta mengine ya mbegu mfano karanga.

Matumizi

hariri

[2] Majimaji ya korosho wakati wa uaandaji wake huwa na asidi muhimu inayotumika hushinda magonjwa mbalimbali yakiwemo ya meno. Pia husaidia kupigana na bacteria ya aina mbalimbali pia sehemu nyingi za za mmea wa korosho hutumiwa na watu wa patammona wa guyona kama dawa.

Magamba ya shina laini huanguliwa na hulowekwa usiku kucha au huchemshwa ili kutibu kuharisha mbegu zikisagwa unga wake hutumiwa kwa kutibu majeraha ya kungatwa na nyoka, mafuta ya korosho pia hutumuka kutibu fangasi za miguu visigino vilivyo katika katika.

Mapishi

hariri

1314.jpg Korosho ni chakula maalumu cha kutafunwa chenye ladha nzuri na hutafunwa huku ikiwa imewekwa chokoleti juu yake, lakini sababu ya gharama yake kubwa korosho haijazoeleka sana kwenye maduka mengi ya vitu vitamu.

Korosho pia hupatikana mara nyingi kwenye mapishi ya thai na China, huliwa nzimanzima na kusagwa na kuliwa kama unga hasa kama kiungo. Huko Malaysia majani huliwa mabichi kama saladi na Brazili korosho hupatikana kwa wingi mno. Maeneo yote wageni hupata kununua korosho zikiuzwa barabarani kwenye paketi ndogo ambazo zimefungwa ndani yake na chumvi kiasi.

Kilevi

hariri

Huko Goa, India, bibo hupondwapondwa kasha kuchanganya na maji na sukari kutengeneza aina ya pombe aina ya Feni(kilevi maarufu) kwa njia ya uchachushaji. Katika mkoa wa kusini mwa Tanzania, Mtwara; bibo hukaushwa na huwekwa baadae huchanganywa na maji na huchachushwa kasha huchuja na kupata pombe kali sana, inayofahamika kwa jina la asili, Gongo. Na huko Msumbiji ni kawaida sana kwa wakulima korosho kutengeneza pombe kali sana kwa kutumia bibo pombe iitwayo “agua ardente” , yaani maji yanayounguza husaidia kuwapa kipato zaidi hasa wajane kwa kuuza pombe hiyo kwa kikombe, kwa chupa n.k.

Majina ya kawaida

hariri

Acajaiba, acajou, acajé (Tupi), kaju (Urdu, Hindi, Gujarati), acajuiba, alcayoiba, anacarde, anacardier, anacardo, andi parippu (Malayalam), cacajuil, cajou, caju (Portuguese), anacardo, cajueiro, cajuilcasho, cashu, castaña de cajú, marañón (Spanish), gajus (Malay),kajjubee (Konkani) godambi (Kannada), h?t di?u (Vietnamese), jambu, jambu golok, jambu mente, jambu monyet, jambu terong, kacang mede, kacang mete (Indonesian), jeedi pappu (Telugu), jocote de marañón, kadju (Sinhala), kasoy (Tagalog), marañón, merey, mundhiri paruppu, sarsgorilla (Tamil), noix d’acajou, pajuil, pomme, pomme cajou, mamuang himmaphan (Thai), korosho (Kiswahili), indijski orah (Serbian), indijski orešcek and akažu (Slovenian).

young fruit.JPG cashew.JPG cashew.JPG

Uzalishaji

hariri

Kwenye mwaka 2016 wazalishaji wakubwa duniani walikuwa: [2]

Nafasi Nchi Mazao ya korosho kwa t
1   Vietnam 1.221.007
2   Nigeria 958.860
3   India 671.000
4   Côte d'Ivoire 607.300
5   Philippines 216.398
6   Tanzania 195.140
7   Mali 164.151
8   Guinea-Bissau 153.888
9   Indonesia 130.072
10   Benin 125.728
Dunia 4.898.210

Tanbihi

hariri
  1. Uanishaji wa kisayansi:Kingdom: Plantae (unranked): Angiosperms (unranked): Eudicots (unranked): Rosids Order: Sapindales Family: Anacardiaceae Genus: Anacardium
  2. Takwimu ya FAO kuhusu mazao duaniani, iliangaliwa Januari 2018

Viungo vya nje

hariri
 
Wikimedia Commons ina media kuhusu: