Wilaya ya Monduli
Wilaya ya Monduli ni kati ya wilaya saba za Mkoa wa Arusha yenye postikodi 23400.
Katika sensa ya mwaka 2012, idadi ya wakazi wa Wilaya ya Monduli ilihesabiwa kuwa 158,929. Katika ile ya mwaka 2022 walihesabiwa 227,585 [1].
Wilaya hii iko katika kaskazini mashariki ya Tanzania. Imepakana na Kenya upande wa kaskazini, Mkoa wa Kilimanjaro na Wilaya ya Arusha Vijijini upande wa mashariki, Mkoa wa Manyara upande wa Kusini na Wilaya ya Ngorongoro pamoja na Wilaya ya Karatu upande wa magharibi.
Historia
haririJina "Monduli" linasemekana kututoka kwa mmoja mzee wa Masai aliyeitwa "Monduli" na kukaa katika eneo la kata ya Monduli Juu wakati wa ukoloni wa Kijerumani.
Utawala
haririWilaya ya Monduli ilikuwa sawa na Jimbo la Uchaguzi la Monduli wakati wa uchaguzi wa bunge. Eneo limegawiwa kwa kata 15 na 51 vijiji au mitaa ya mjini. Eneo lote ni kilomita za mraba 6,419.
Makao makuu ya wilaya iko Monduli Mjini ambayo ni moja wa miji midogo miwili (pamoja na Namanga) katika wilaya yenye tabia ya vijijini.
Jiografia
haririMonduli iko upande wa magharibi wa Jiji la Arusha na Mlima Meru. Sehemu kubwa ya eneo lake ni milima pamoja na volkeno ya Oldoinyo Lengai iliyokatwa na Bonde la Ufa. Pia mlima karibu na Monduli mjini huitwa Monduli, ni volkeno bwete.
Marejeo
haririViungo vya Nje
hariri- http://legacy.lclark.edu/~peck/EAf-Orient/Tanzania/T-independence.htm Archived 2009-07-27 at Archive.today
- http://www.arusha.go.tz/english/Pages/Health/index.php Archived 2013-04-18 at Archive.today
- http://www.parks.it/world/TZ/parchi.arusha/Epar.html
- http://www.infohub.com/TRAVEL/SIT/sit_pages/18500.html
- http://www.trazzler.com/trips/the-maasai-red-market-at-monduli-juu-in-arusha-tanzania-tz Archived 2013-02-04 at Archive.today
- "educ".
- http://www.infojep.com/culturaltours/monduli_juu_brochure.html
- http://www.ieftz.org
Kata za Wilaya ya Monduli - Mkoa wa Arusha - Tanzania | ||
---|---|---|
Engaruka | Engutoto | Esilalei | Lashaine | Lemooti | Lepurko | Lolkisale | Majengo | Makuyuni | Meserani | Mfereji | Migungani | Moita | Monduli Juu | Monduli Mjini | Mswakini | Mto wa Mbu | Naalarami | Selela | Sepeko |
Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Arusha bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Wilaya ya Monduli kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |