Ololosokwan ni kata ya Wilaya ya Ngorongoro katika Mkoa wa Arusha, Tanzania, yenye postikodi namba 23709.

Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi walihesabiwa 16,503 [1]. Wakati wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 6,557[2].

Kata hiyo imepakana na jamhuri ya Kenya kwa upande wa kaskazini, hifadhi ya taifa ya Serengeti kwa upande wa magharibi na kata ya Soitsambu kwa upande wa kusini.

Kata ya Ololosokwan ina vijiji viwili, Ololosokwan na Njoroi. Ololosokwan imeundwa na vitongoji vitatu ambavyo ni Sero, Mairowa na Ololo juu.

Asilimia 98 ya wakazi wa kata ya Ololosokwan ni wafugaji wa kabila la Wamasai. Ni kata yenye wasomi wengi katika tarafa ya Loliondo.

Jina la "Ololosokwan" limetokana na kuwepo kwa nyati wengi katika sehemu hiyo (nyati kwa lugha ya Kimasai anaitwa Olosokwan, hivyo jina Ololosokwan lina maana "Yenye Nyati").

Marejeo

hariri
  1. https://www.nbs.go.tz
  2. "Sensa ya 2012, Arusha - Ngorongoro DC" (PDF). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2016-03-03. Iliwekwa mnamo 2016-05-20.
  Kata za Wilaya ya Ngorongoro - Mkoa wa Arusha - Tanzania  

Alailelai | Alaitolei | Arash | Digodigo | Enduleni | Engaresero | Enguserosambu | Eyasi | Kakesio | Kirangi | Maalon | Malambo | Misigiyo | Nainokanoka | Naiyobi | Ngoile | Ngorongoro | Olbalbal | Oldonyosambu | Oloipiri | Olorien/Magaiduru | Ololosokwan | Orgosorok | Pinyinyi | Piyaya | Sale | Samunge | Soitsambu


  Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Arusha bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Ololosokwan kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.