Wilfred Moriasi Ombui
Wilfred Ombui Moriasi ni mwanasiasa wa Kenya, mwanachama wa Chama cha KANU. Miaka 2009-2013 alikuwa mbunge akiwakilisha eneo bunge la Mugirango Kaskazini kwa tikiti ya Chama cha KANU[1]
Historia
haririOmbui alizaliwa katika kijiji cha Bonyunyu karibu na Kenyoro, Kata ya Itibo, Tarafa ya Ekerenyo, Wilaya ya Nyamira Mkoa wa Nyanza nchini Kenya
Elimu
haririAlisoma katika Shule ya Msingi ya ELCK Kenyoro kabla ya kujiunga na Shule ya Upili ya Kisii.
Kazi zingine
haririKando na kuwa mwalimu wa Shule ya Msingi, Ombui pia anajulikana na wengi kwa kuwa meneja wa Chama cha walimu cha Mwalimu SACCOS tawi la Gusii kwa muda Mrefu.
Siasa
haririAlijitosa ulingoni mwa siasa kwa mara ya kwanza wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu wa 2007. Umaarufu wake ulizambaa haraka na akakishinda kiti hicho cha Ubunge huku akiwashinda wapinzani wake akiwemo mtangulizi wake Godfrey Okeri Masanya na Mwanasheria Joseph Kiangoi Ombasa.
Tazama pia
haririAlitanguliwa na Godfrey Masanya Okeri |
Mbunge wa Mugirango Kaskazini 2007- |
Akafuatiwa na _ |
Marejeo
hariri- ↑ Members Of The 10th Parliament Ilihifadhiwa 16 Juni 2008 kwenye Wayback Machine.. Bunge la Kenya. Accessed 19 Juni 2008.
Makala hii kuhusu mwanasiasa huyu wa Kenya bado ni mbegu. Unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuongezea habari. |