Uchaguzi Mkuu wa Kenya, 2007
Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2007 nchini Kenya ulikuwa na matatizo mengi na kusababisha machafuko yaliyopelekea kutokea kwa vifo. Katika kadhia hii, watu 1,300 walipoteza maisha na wengine 300,000 kujeruhiwa.[1]
Jamhuri ya Kenya |
Makala hii imepangwa kwa mfululizo: |
|
Nchi zingine · Atlasi |
Baada ya Raila Odinga wa ODM kuongoza katika hesabu ya kura kwa muda mrefu Tume ya Uchaguzi ya Kenya lilisimamisha hesabu kwa muda wa usiku mmoja na baada ya kuanza upya kura za Mwai Kibaki wa PNU zilikuwa mbele. Tume ikamtangaza Kibaki kuwa mshindi naye aliapishwa mara moja bila kusubiri muda wa kisheria kwa malalamiko. Watazamaji waliona kasoro, makosa na matokeo yaliyodokeza ya kwamba hesabu ya kura ilibadilishwa kwenye ngazi za kupiga jumla za kura kimkoa na kitaifa. Vilevile kuna madokezo ya kwamba kura za kirais ziliongezwa katika usiku ambako hesabu ilisimamishwa.
Matokeo yaliyotangazwa ni kama yafuatayo:
- Mwai Kibaki: kura 4,584,721 (asilimia 46.7)
- Raila Odinga: kura 4,352,993 (asilimia 44.3)
- Kalonzo Musyoka: kura 879,903 (asilimia 9)
Wagombea wengine walimaliza kwa kura chache tu.
Uchaguzi wa Bunge 2007
hariri- Tazama Uchaguzi wa bunge nchini Kenya, 2007 kwa matokeo ya kila jimbo
Wabunge 207 walichaguliwa. Kura zitarudiwa katika majimbo 3. Wabunge 12 wa ziada watateuliwa na rais. Akifuata kawaida atawateua kufuatana na nguvu ya vyama bungeni.
- PNU na vyama vinavyoshirikishwa nayo vina viti 78 (PNU 43, KANU 16, vyama vingine 21)
- ODM na chama shirikishwa cha NARC vina viti 102 (ODM pekee 99).
- ODM-Kenya ina viti 16.
- Wabunge 11 walichaguliwa kwa majina ya vyama vidogo visivyoshirikishwa na vyama vikubwa.
Magazeti yalitoa taarifa ya kwamba wabunge 30 wa vyama vidogo waliunda "Kundi la vyama vidogo bungeni" (Small Parties Parliamentary Group); idadi hii ingejumlihsa wabunge waliohesabiwa juu kama kundi la PNU.
ODM | NARC ilishirikishwa na ODM |
PNU | Vyama shirikishwa vya PNU |
KANU Chama chirikishwa na PNU |
ODM-Kenya | Wabunge wanaojitegemea | JUMLA | |
---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Wabunge | 99 | 3 | 43 | 21 | 14 | 16 | 11 | 207(of 210) |
Vyama shirikishwa vya PNU- KANU (14), Sisi Kwa Sisi (2), Safina (5), NARC-Kenya (4), FORD-Kenya (1), Ford-P (3), New Ford-K (2), Mazingira Party (1), Ford-A (1), DP (2) Wabunge wa kujitegemea waliingia kupitia vyama vidogo kama PDP (1), PPK (1), NLP (1), KADDU (1), UDM (1), PICK (1), CCU (1), Kenda (1) |
Tanbihi
hariri- ↑ "ICC inaashiria kupata nafasi ya kuwakabili watuhumiwa wa vurugu za uchaguzi nchini Kenya – DW – 31.07.2009". dw.com. Iliwekwa mnamo 2024-11-01.