Bill Gates
Bill Gates (jina kamili: William Henry Gates III; alizaliwa 28 Oktoba 1955) ni mwanzilishi wa kampuni ya Microsoft, mtu tajiri wa pili duniani na mwanzilishi wa asasi isiyo ya kiserikali ya Bill and Melinda Gates Foundation.
Bill Gates | |
---|---|
| |
Alizaliwa | 28 Oktoba 1955 |
Nchi | Marekani |
Kazi yake | mwanzilishi wa kampuni ya Microsoft |
Makala haina vyanzo vya kutosha
Makala (au sehemu ifuatayo ya makala) inatoa habari bila kuonyesha vyanzo au uthibitisho wowote.
|
Bill Gates ni mwanzilishi, mwenyekiti na mbunifu mkuu wa programu za kampuni ya Microsoft, kampuni ya programu yenye mafanikio zaidi duniani, inayoaminika kwa utengenezaji wa programu zilizo na nguvu na ubunifu hali zikiwa bado zenye utumizi mwepesi. Microsoft sasa inaajiri zaidi ya watu elfu hamsini na tano katika nchi themanini na tano.
William Gates III alizaliwa na kulelewa katika mji wa Seattle pamoja na dada zake wawili. Katika umri mdogo Bill Gates alivutiwa na utengenezaji wa programu akiwa katika mojawapo wa shule kijijini Seattle. Akiwa huko shuleni Seattle, Bill Gates alikutana na Paul Allen, mwanafunzi mwenzake wakawa marafiki. Hapo ndipo wakaanza kutumia tarakilishi ndogo ya shule kujiendeleza ujuzi wao.
Walijiunga na kampuni ya kompyuta, malipo yao ikiwa ni kutumia tarakilishi yenye nguvu zaidi. Kazi yao ilikuwa ni kutafuta nukshi katika mitambo ya kompyuta, wakati huohuo waliweza kijifunza lugha mpya za kompyuta. Bill akaenda kwenye Chuo Kikuu cha Harvard. Kwa mara nyingine tena akajiunga pamoja na Paul kuandika toleo jipya la programu ya Msingi wa lugha ya kwanza ya kompyuta ya kibinafsi, iitwayo Altair 8800. Kampuni hiyo iliridhishwa na kazi ambayo Bill Gates na Paul Allen waliofanya na programu hiyo ikapewa leseni. Jambo hili liliwachangia Gates na Allen kuanzisha kampuni ya Microsoft, iliyokuwa ikitengenezea kampuni zingine programu. Bill Gates aliacha masomo yake katika chuo kikuu cha Harvard na kujishughulisha muda wake wote katika biashara.
Mapumziko yao yalikuja walipotengeneza mfumo wa kuendesha kompyuta uitwao MS-DOS uliotumika katika kompyuta ya kwanza ya kibinafsi ya IBM. Baadaye waliweza kuzishawishi kampuni zingine zinazotengeneza kompyuta kutumia mfumo huo wa MS-DOS. Mfumo huu mpya wa MS-DOS ulipata umaarufu katika soko miaka ya 1980 na baadaye, Microsoft pia ilianza kutengeneza programu kama vile neno sindikizi.
Microsoft ilitangaza mfumo mpya wa uendeshaji wa kompyuta uitwao Windows 1.0 mwaka wa 1983, ambao ulikuwa na grafiksi bora na pia uliwezesha kufanya zaidi ya jambo moja kwa wakati mmoja. Hata hivyo hakuwa bidhaa nyingine iliyotolewa miaka mbili baadaye hadi mwaka wa 1985, kwa kuwa ni programu chache zilizoweza kuendeshwa katika mfumo huu wa Windows 1.0. Hivyo mfumo huu mpya haukupata umaarufu vile.
Kipindi cha miaka mitano baadaye Microsoft ilitoa mifumo mipya ya Windows 2.0 iliyokuwa bora zaidi kuliko mifumo ya hapo awali. Kampuni ya Microsoft iliweza kupata umaarufu zaidi katika soko la hisa, na akiwa umri wa miaka 31, Bill Gates aliweza kuwa bilionea mchanga zaidi katika historia ya Marekani.
Katika mwaka wa 1990 Microsoft ikiongozwa na Bill Gates ilitoa toleo jipya la Windows liitwayo Windows 3.0 na kuboreshwa kiasi GUI. Toleo hili jipya liliweza kuuzwa zaidi ya nakala milioni kumi, likifuatiwa na matoleo mengine ya Windows 3.1, 3.11 na makundi ya kazi ambayo yaliongeza misaada kwa mitandao. Kutokana na mafanikio yao ya maendeleo, Microsoft ilitoa matoleo mengine ya Windows 95 ikifuatiwa na Windows 98, 2000, Millennium Edition na toleo la sasa Windows XP. Kila toleo jipya lilipotolea kampuni ya Microsoft ilizidi kupata umaarufu katika soko la hisa, ikiongezwa na baadhi ya programu kama vile Microsoft Office, michezo n.k. Umaarufu huu umemfanya Bill Gates kuwa mtu tajiri duniani myenye thamani ya wastani wa dola bilioni arubaini na sita.
Bill Gates pia ana maslahi katika biashara nyingine akiwa na nafasi nyingi za uwekezaji na vyeo katika kampuni tofauti ikiwemo Corbis Corporation, Berkshire Hathaway Inc, Teledesic Corporation. Mwaka wa 1998 Gates alijitoa jukumu lake kama Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya Microsoft na kuzingatia maendeleo ya teknolojia na bidhaa mpya.
Bill Gates alifanya ndoa na Melinda French Gates mwaka wa 1994 na wakabarikiwa na watoto watatu, Jennifer, Rory na Fibi. Wote wawili Bill na Melinda ni waanzilishi wa mashirika yasiyo ya kiserikali. Waliweza kulianzisha shirika la Bill na Melinda Gates Foundation ambalo limeweza kuchangia zaidi ya dola bilioni tatu nukta mbili kuboresha afya duniani, dola bilioni mbili kuboresha fursa ya masomo kwa familia zisizojiweza. Zaidi ya hayo limeweza pia kuchangia dola milioni mia nne sabini na saba kwa miradi ya jamii na zaidi ya dola milioni mia nne themanini na nane kwa miradi maalum na kampeni za kuhamasisihwa kila mwaka.
Ubunifu wa Bill Gates wa kutengeneza programu umekuwa mchango wake katika mapinduzi ya kompyuta na sayansi ya kompyuta.
Viungo vya nje
hariri- Blogu ya Bill Gates
- Tovuti ya kampuni ya Bill Gates ya Microsoft
- Taasisi ya Bill and Melinda Gates Foundation
Makala hii kuhusu mwanasayansi fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Bill Gates kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |