WorldCat ni jina la hazinadata kubwa zaidi duniani kuhusu vitabu vinavyopatikana katika maktaba elfu kadhaa kote duniani.

WorldCat ni kifupi cha "world catalogue" yaani orodha (ya vitabu) ya kimataifa.

Historia

hariri

Ilianzishwa mwaka 1967 wakati maktaba za jimbo la Ohio, Marekani ziliungana kuunda taasisi ya "Ohio Computer Library Center" (OCLC) kwa shabaha ya kupeana habari za vitabu vilivyopatikana katika maktaba za vyuo 54 vya Ohio.

Tangu mwaka 1978 maktaba za majimbo mengine ya Marekani yalikubaliwa na jina kubadilishwa kuwa "Online Computer Library Center".

Tangu mwaka 2002 kila maktaba duniani inaweza kujiunga na OCLC. Mwaka 2019 kulikuwa na maktaba wanachama 17,983 katika nchi 123 tofauti.[1]

Huduma

hariri

Ukitafuta kitabu kwenye WorldCat itakupa majina ya maktaba wanachama ambamo kitabu hicho kinapatikana. Kama hakuna maktaba iliyo karibu yenye kitabu hicho unaweza kuazima kitabu (karatasi au online) kama maktaba yako ni mwanachama ya WolrdCat na kukubali kuazima kutoka maktaba nyingine.

WolrdCat inatoa pia nafasi ya kupata habari zinazohitajika kwa dondoo kwa kubofya "Cite/Export" (copy a citation).

Maktaba wanachama katika Afrika ya Mashariki[2]

hariri

(zote ziko Nairobi kama mahali pengine hapatajwi)

  • Kenya Education Management Institute
  • Kenya Institute of Education
  • Kenya Institute of Management
  • Kenya Institute of Management, The
  • Kenya Maritime Authority , Mombasa
  • Kenya Methodist University
  • Herufi House
  • Kenya National Library Services - Buruburu
  • Kenya Power & Lighting Co
  • Kenya School of Law

(zote ziko Dar es Salaam kama mahali pengine hapatajwi)

  • Family History Center,
  • University of Dar Es Salaam
  • African Court on Human and Peoples' Rights
  • Bank of Tanzania Training Institute Library
  • Hamilton Tutorial College
  • ILO Office In Dar es Salaam
  • Main Library; The Eastern Africa Statistical Training Centre
  • Millenium Academy, Nyamagana Mwanza
  • Muhimbili University of Health and Allied Sciences
  • National Institute for Medical Research

(zote ziko Kampala kama mahali pengine hapatajwi)

  • Uganda Bible Institute, Mbarara
  • Uganda Christian University, Mukono
  • Uganda Management Institute
  • Uganda Martyrs University
  • Jinja Uganda Family History Center, Jinja
  • Kampala Uganda Family History Center
  • Ministry of Finance, Planning and Economic Development Resource Centre
  • National Library of Uganda

Tanbihi

hariri
  1. About OCLC, iliangaliwa Aprili 2019
  2. WorldCat find a library

Marejeo ya Nje

hariri
  • Wendy M. Grossman (21 Januari 2009). "Why you can't find a library book in your search engine: Finding a book at your local library should just involve a simple web search; but thanks to a US cataloguing site, that is far from the case". The Guardian.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  • WorldCat Tovuti rasmi
  • WorldCat Identities
  • What is OCLC?