Yakobo wa Moutiers
Yakobo wa Moutiers (kwa Kifaransa: Jacques de Tarentaise; Asiria, Mesopotamia Kaskazini, karne ya 4 - 16 Januari 429) alikuwa askofu wa kwanza wa mji huo katika Savoie, Ufaransa wa leo.
Kabla ya kubatizwa alikuwa askari wa jeshi la Uajemi. Baada ya kukutana na Honorati wa Arles akawa mmonaki huko Lerins. Honorati alipochaguliwa kuwa askofu mkuu, akamfanya Yakobo askofu ili kueneza Ukristo[1].
Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.
Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 16 Januari[2].
Tazama pia
haririTanbihi
haririMarejeo
hariri- Marius Hudry, Histoire des communes savoyardes : Albertville et son arrondissement (vol. 4), Roanne, Éditions Horvath, 1982, 444 p. (ISBN 978-2-7171-0263-5).
- Jacques Lovie, Histoire des diocèses de France : Chambéry, Tarentaise, Maurienne, vol. 11, Paris, Éditions Beauchesne, 1979, 299 p. (ISSN 0336-0539).
- Denise Péricard-Méa, Éric Deschamps, « En Tarentaise, un saint Jacques concurrent de Compostelle ? Un patrimoine et une histoire sauvés de l’oubli », SaintJacquesInfo, février 2016.
Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |