Yehoyakimu
Jehoyakimu (kwa Kiebrania יְהוֹיָקִים, Yehoyakim, "Yule ambaye YHWH amemuinua") (635 KK - 597 KK) alikuwa mtu wa ukoo wa Daudi aliyetawala ufalme wa Yuda kwa miaka 11 (608 KK hadi kifo chake).
Mwana wa mfalme Yosia, kabla ya kutawazwa na Farao Neko II , aliitwa Eliakimu (אֶלְיָקִים, Eliakim).
Alikataa kufuata maelekezo ya nabii Yeremia hata akachana na kuchoma maandishi aliyomtumia (Yer 36:1-32).
Alifariki huku mji wa Yerusalemu umezingirwa na jeshi la Nebukadneza wa Babuloni.
Makala hii kuhusu mtu wa Biblia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Yehoyakimu kama habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |