Yevgeniya Polyakova

Yevgeniya Yevgeniyevna Polyakova (alizaliwa 29 Mei 1983 jijini Moscow,[[Urusi) ni mwanariadha wa Urusi aliyebobea katika mbio ya 100m.[1]

Rekodi za medali

Yevgeniya Polyakova
Anawakilisha nchi Urusi
Riadha ya Wanawake
Michezo ya Olimpiki
Dhahabu 2008 Beijing Mbio ya 4 x 100m
Mashindano ya Mabingwa wa Uropa ya Ndani ya Ukumbi
Dhahabu 2009 Torino Mbio ya 60 m
Fedha 2007 Birmingham Mbio ya 60 m

Polyakova aliwakilishwa Urusi katika Olimpiki ya 2008 iliyokuwa Beijing,Uchina.Alishiriki katika mbio ya 100m. Katika awamu ya kwanza ya mbio za kuhitimu,alichukua nafasi ya kwanza mbele ya Jade Bailey wa Barbados na Sherone Simpson wa Jamaika.Alikimbia mbio hiyo kwa muda wa sekunde 11.24 na kuhitimu kuingia awamu ya pili. Katika mbio hiyo aliboresha muda wake ukawa sekunde 11.13 akimaliza nyuma ya Shelly-Ann Fraser wa Jamaika na hivyo basi akahitimu kukimbia katika mbio za nusu fainali. Katika nusu fainali alikimbia kwa muda wa 11.38s,akachukua nafasi ya saba katika mbio hiyo na akashindwa kuhitimu [2] kuingia mbio za fainali. Pamoja na Aleksandra Fedoriva, Yulia Gushchina na Yuliya Chermoshanskaya alishiriki katika mbio ya 4 x 100m. Katika mbio ya kwanza ya kuhitimu,walichukua nafasi ya pili nyuma ya Jamaika lakini mbele ya Ujerumani na Uchina. Muda wao wa sekunde 42.87 pia ulikuwa wa pili kwa kasi kwa jumla katika mataifa 16 yaliyoshiriki katika mbio hiyo. Kutokana na matokeo haya,walihitimu kukimbia katika fainali ambapo walikimbia kwa muda wa 42.31s,wakachukua nafasi ya kwanza na kushinda medali ya dhahabu. Timu ya Jamaika hawakumaliza kutokana na kosa katika kubadilishana. [3]

Mafanikio

hariri
Mwaka Shindano Pahala pa kushindana Matokeo Maelezo
2007 Mashindano ya Mabingwa wa Uropa ya Ndani ya Ukumbi Birmingham, Uingereza 2 Mbio ya 100 m
2008 Mashindano ya Mabingwa wa Dunia ya IAAF ya Ndani ya 2008 Valencia, Uhispania 5 Mbio ya 60 m

Muda bora za binafsi

hariri
  • Mbio ya mita 60 - 7.09 s (2008, mbio ya ndani ya ukumbi)
  • Mbio ya mita 100 - 11.09 s (2007)

Marejeo

hariri
  1. Yevgeniya Polyakova

Viungo vya nje

hariri