Barbadosi
(Elekezwa kutoka Barbados)
Barbadosi ni nchi ya kisiwani katika Bahari ya Karibi takriban 430 km kaskazini - mashariki kwa Venezuela (Amerika Kusini).
| |||||
Kaulimbiu ya taifa: "Pride and Industry" | |||||
Wimbo wa taifa: In Plenty and In Time of Need | |||||
Mji mkuu | Bridgetown | ||||
Mji mkubwa nchini | Bridgetown | ||||
Lugha rasmi | Kiingereza | ||||
Serikali | Jamhuri Sandra Mason Mia Mottley | ||||
Uhuru kutoka Uingereza |
30 Novemba 1966 | ||||
Eneo - Jumla - Maji (%) |
431 km² (ya 199) Kidogo sana | ||||
Idadi ya watu - [[]] kadirio - 1010 sensa - Msongamano wa watu |
(ya 181) 277,821 660/km² (ya 15) | ||||
Fedha | Barbados dollar ($) (BBD )
| ||||
Saa za eneo - Kiangazi (DST) |
(UTC-4) (UTC) | ||||
Intaneti TLD | .bb | ||||
Kodi ya simu | +1-246
- |
Nchi jirani za karibu kuvukia bahari ni Saint Lucia na Saint Vincent upande wa magharibi, Trinidad na Tobago upande wa kusini na Grenada upande wa kusini-magharibi.
Barbados ni kisiwa cha Antili Ndogo. Kwa urefu kinafikia km 34 na kwa upana 23.
Wakazi ni 277,821, na kwa asilimia 91 wana asili ya Afrika, 4% ya Ulaya, 1% ya India.
Lugha rasmi ni Kiingereza, ingawa wakazi wengi kabisa wanaongea kwa kawaida aina ya Krioli inayoitwa Kibajan.
Upande wa dini, 75.6% ni Wakristo, hasa Waanglikana (23.9%) na Wapentekoste (19.5%). Dini nyingine kwa pamoja zinafikia 3%, kwa kuwa 21% hawana dini yoyote.
Tazama pia
haririMakala hii kuhusu maeneo ya Bahari ya Karibi bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Barbadosi kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |