Yohane Mbatizaji Garcia
Yohane Mbatizaji Garcia (Almodóvar del Campo, Ciudad Real, Hispania, 10 Julai 1561 - Cordoba, Hispania, 14 Februari 1613) alikuwa padri wa Kanisa Katoliki na mtawa wa shirika la Watrinitari, yaani watawa wa Utatu mtakatifu, waliojitoa kabisa kwa ajili ya kukomboa Wakristo waliotekwa utumwani.
Alijitahidi kufanya urekebisho wa shirika hilo kwa kuanzisha tawi la Watrinitari Peku kwa kufuata mfano wa Teresa wa Yesu kati ya vipingamizi vikubwa na tabu nyingi.
Pia aliandika vitabu vingi vya teolojia.
Alitangazwa na Papa Pius VII kuwa mwenyeheri tarehe 26 Septemba 1819, halafu Papa Paulo VI alimtangaza mtakatifu tarehe 25 Mei 1975[1].
Tazama pia
haririTanbihi
hariri- ↑ "Saint John Baptist of the Conception". Santi e Beati. Iliwekwa mnamo 22 Julai 2015.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Martyrologium Romanum
Viungo vya nje
hariri- Hagiography Circle Archived 9 Februari 2021 at the Wayback Machine.
Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |