Zakaria Kibona
Zakaria Kibona (amezaliwa 14 Machi 1990 mjini Dar es Salaam) ni mchezaji wa mpira wa miguu kutoka nchini Tanzania, ambaye kwa sasa anaichezea klabu ya Atlantis FC inayoshiriki katika ligi ya pili ya Ufini katika mji mkuu wa Helsinki nchini Ufini.
Zakaria Kibona | ||
Maelezo binafsi | ||
---|---|---|
Jina kamili | Zakaria Kibona | |
Tarehe ya kuzaliwa | 14 Machi 1990 | |
Mahala pa kuzaliwa | Dar es salaam, Tanzania | |
Urefu | mita 180 | |
Nafasi anayochezea | Mshambuliaji | |
Maelezo ya klabu | ||
Klabu ya sasa | Atlantis FC | |
Namba | 14 | |
Klabu za vijana | ||
Atlantis FC | ||
Klabu za ukubwani | ||
Miaka | Klabu | |
2008 | Atlantis FC | |
Timu ya taifa | ||
2000-2004 2004- 2006- |
Tanzania U-15 Tanzania U-17 Tanzania | |
* Magoli alioshinda |
Kuanza kwake mpira UfiniEdit
Zakaria ni mshambuliaji matata wa katika kati ambae alijiunga na Atlantis FC ya vijana mwaka 2002 na alicheza na klabu hiyo hadi mwaka 2007 baada ya kocha wa klabu ya Atlantis FC ya watu wakubwa kuomba apandishwe katika timu ya wakubwa na baadae alionekana kua ni mchezaji mzuri ambae kwa sasa anacheza mechi nyingi nakua kiungo muhimu wa timu hiyo.
Timu ya taifa ya TanzaniaEdit
Bwana Zakaria Kibona aliichezea timu ya taifa ya Tanzania ya vijana wa umri mdogo ya myaka 15 na myaka 17 kabla ya mwaka 2006 kuitwa kuichezea timu ya taifa ya Tanzania ya watu wakubwa na kwa sasa anamechi 15 na timu ya taifa hiyo ya Tanzania.
Uraia wakeEdit
Zakariba Kibona ana uraia wa nchi ya Tanzania na Ufini na alipata uraia wa Ufini kwani mchezaji huyo alienda Ulaya akiwa na umri mdogo nakukaa huko muda mrefu, na sio yeye tu ambae alichukua uraia katika wachezaji mpira kuna wachezaji mashuhuri ambao walichukua uraia kutokana na maslahi yao fulani kama kulipa ushuru au mengine na baadhi yao ni kama vile Ronaldinho, Samuel Eto'o na wengine pia.
ZawadiEdit
Kuchukua ubingwa pindi alipokua akichezea Atlantis FC ya vijana mwaka 2006 katika mashindano ya vijana.