Samuel Eto'o

Mchezaji soka wa zamani wa Kamerun

Samuel Eto'o Fils (alizaliwa 10 Machi 1981) ni mchezaji wa soka wa Kameruni ambaye anacheza kama mshambuliaji kwa Qatar SC.

Samuel Eto'o
Eto'o mwaka 2011
Maelezo binafsi
Jina kamiliSamuel Eto'o
tarehe ya kuzaliwa10 Machi 1981 (1981-03-10) (umri 43)
mahali pa kuzaliwaDouala, Cameroon
Senior career*
MiakaTimuApps(Gls)
1997–2000Real Madrid3(0)
1997–1998Leganés (mkopo)28(3)
1999Espanyol (mkopo)0(0)
2000Mallorca (mkopo)13(6)
2000–2004Mallorca120(48)
2004–2009Barcelona144(108)
2009–2011Inter Milan67(33)
2011–2013Anzhi Makhachkala53(25)
2013–2014Chelsea21(9)
2014–2015Everton14(3)
2015Sampdoria18(2)
2015–2018Antalyaspor76(44)
2018Konyaspor13(6)
2018–2019Qatar SC17(6)
Total587(293)
Timu ya Taifa ya Kandanda
2000Cameroon U236(1)
1997–2014Cameroon118(56)
Teams managed
2015–2016Antalyaspor (meneja wa muda)
* Senior club appearances and goals counted for the domestic league only.
† Appearances (Goals).

Ndiye mchezaji aliyependekezwa zaidi kuwa bora kati ya wale wa Kiafrika wa wakati wote, baada ya kushinda tuzo ya mchezaji wa mwaka wa Afrika mara nne: mwaka 2003, 2004, 2005 na 2010. Alikuwa wa tatu katika tuzo ya FIFA World Player ya Mwaka mwaka 2005.

Eto'o alifunga magoli zaidi ya 100 katika msimu wa tano na Barcelona, na pia ni mmiliki wa rekodi katika idadi ya maonyesho na mchezaji wa Afrika huko La Liga. Mwaka 2010, alikuwa mchezaji wa kwanza kushinda mafanikio mawili ya bara ya Ulaya. kufuatia mafanikio yake ya nyuma ya Barcelona na Inter Milan. Yeye ni mchezaji wa pili katika historia ya kupiga fainali mbili za Kombe la Mabingwa wa UEFA na mchezaji wa nne, baada ya Marcel Desailly, Paulo Sousa na Gerard Piqué, kushinda nyara miaka miwili mfululizo na timu tofauti.

Mnamo Septemba 2021, Samuel Eto'o, alitangaza kugombea urais wa Shirikisho la Soka la Cameroon (Fecafoot).

Samwel Eto'o anamiliki mitandao ya simu za mkononi huko kwao Kamerun.

Kazi ngazi ya Klabu

hariri

Real Madrid

hariri

Akiwa mwanafunzi wa Akademi ya Kadji Sports Academy kutokea nchini Kameruni, Eto'o alijiunga na akademi ya vijana ya Real Madrid mwaka 1997, lakini aliweza tu kufanya mazoezi na Real Madrid Castilla/Real Madrid B, kwani alikua bado mdogo.[1] Real Madrid B walishushwa daraja hadi ligi ya tatu (Segunda División B), ambapo wachezaji wasio raia wa Umoja wa Nchi za Ulaya (EU) hawaruhusiwi kucheza, na matokeo yake alihamishwa kwa mkopo kwenda CD Leganés klabu ya ligi daraja la pili, kwa msimu wa 1997–98.[2] Baada ya kucheza mechi 30 na kufunga mabao manne pekee, alirudi Madrid mwishoni mwa msimu wa 1998–99. Mnamo Januari 1999, alipelekwa kwa mkopo klabu ya RCD Espanyol[3], lakini alicheza mechi moja dhidi ya Real Valladolid kwenye mashindano ya Copa del Rey.

Mallorca

hariri

Msimu uliofuata, katika dirisha la usajili la majira ya baridi, alihamia kwa mkopo klabu ya Mallorca inayoshiriki ligi kuu ya Hispania (La Liga), ambako alifunga mabao sita kwenye mechi 19. Mwishoni mwa msimu, Eto'o aliachana na Real Madrid na kusaini mkataba wa kudumu na Mallorca kwa ada ya uhamisho ya Euro milioni 4.4 iliyoweka rekodi. Katika msimu wake wa pili, alifunga mabao 11 na kuanza kuvutia timu mbalimbali katika ligi nzima. Rais wa Mallorca, Mateo Alemany, alielezea kuhusu mtindo wake wa uchezaji, "Sidhani kama kuna mchezaji mwingine duniani ambaye angewapendeza mashabiki zaidi kwa sasa." Eto'o mwenyewe alizungumzia kuhusu kupanda kwake chati, "Ninapenda kuwa hapa Mallorca; nimekuwa nikitunzwa vizuri kila wakati, mashabiki wananithamini, na pia nina mkataba hadi mwaka 2007." Alionyesha shukrani kwa mashabiki alipotoa msaada wa chakula cha thamani ya €30,000 kwa mashabiki wa Mallorca waliokuwa wamesafiri kuhudhuria fainali za Copa del Rey mwaka 2003 dhidi ya Recreativo de Huelva. Mallorca walishinda mechi hiyo 3–0, huku Eto'o akifunga mabao mawili ya mwisho yaliyohakikisha ushindi. Eto'o pia alifunga katika ushindi wa ugenini mara mbili mfululizo dhidi ya klabu yake ya zamani Real Madrid: mchezo wa kwanza, kwenye kipigo cha 1-5, ukiwa ndio mchezo pekee kwa Madrid kupoteza msimu wa 2002-03 waliposhinda taji la msimu;[4] mchezo wa pili ulimalizika 2-3 matokeo ambayo yaliwazuia Real Madrid kushinda taji la ligi mfululizo.[5]

Barcelona

hariri

2004–07: Uhamisho, Tuzo ya Pichichi na Kombe la Kwanza la Ligi ya Mabingwa Ulaya

hariri
 
Eto'o akisherehekea bao akiwa na Barcelona mwezi Disemba 2005

Eto'o aliondoka Mallorca akiwa mfungaji bora wa muda wote wa klabu hiyo kwenye ligi ya ndani (mabao 54) alipohamia Barcelona katika majira ya joto ya mwaka 2004 kwa ada ya uhamisho ya Euro milioni 24, baada ya mazungumzo ya muda mrefu ya ikizihusisha Mallorca na Madrid. [6] Awali, raisi wa Real Madrid, Florentino Perez alitaka kununua haki za mauzo za mchezaji huyo ili kumtoa kwa mkopo tena. Ofa ya Barcelona ililenga wazi kutaka kumnunua[7]. Hata na hivyo, Madrid ilishafikia kiwango cha idadi ya wachezaji wasio wa Jumuiya ya nchi za Ulaya (3) kilichotakiwa kwa klabu za bara Ulaya. Eto'o alicheza mechi yake ya kwanza akiwa na Barcelona katika ufunguzi wa msimu dhidi ya Racing de Santander tarehe 29 Agosti 2004. Baada ya kushinda taji la La Liga msimu wa 2004-05, Barcelona waliandaa sherehe kubwa kwenye uwanja wao wa Camp Nou, wakati wa sherehe hizo, Eto'o aliwahamasisha mashabiki kwa kusema, "Madrid, cabrón, saluda al campeón" (kwa Kiingereza, "Madrid, bastards, salute the champions"). Shirika la mpira wa miguu la Hispania lilimtoza Etoo faini ya Euro 12,000 kwa matamshi hayo ambayo baadae aliomba radhi kwa kitendo hicho. Alionyesha wazi kujitia kitendo chake na kuomba radhi kwani Madrid ndio ilikua klabu yake ya kwanza kwenye soka la kulipwa. Kiongozi wa mashabiki wa Madrid hakuonyeshwa kuridhishwa na radhi ya Etoo, na alinikuliwa akisema “Mchezaji huyu ni mahiri sana, lakini ana mapungufu makubwa kama mtu binafsi."[8] He signed an improved contract with Barcelona in June 2005.[9]

Baada ya kukosa tuzo ya Pichichi kwa msimu uliopita, ambayo hutolewa kwa mfungaji bora wa La Liga, Eto'o alishinda tuzo hiyo msimu uliofuata baada ya kumzidi mshambuliaji wa Valencia David Villa siku ya mwisho ya msimu tarehe 20 Mei 2006 alipopachika bao lake la 26 la msimu dhidi ya Athletic Bilbao. Eto'o pia alifunga mabao sita katika kampeni ya Barcelona ya kushinda taji la UEFA 2005-06. Kwenye fainali ya UEFA 2006, mlinda mlango wa Arsenal Jens Lehmann alitolewa kwa kadi nyekundu mwanzo ni mwa mchezo kwa kumwangusha Eto'o nje kidogo ya eneo la hatari, lakini timu ya Barcelona ilisumbuka kutumia faida ya mchezaji pungufu kwa wapinzani Eto'o alipofunga bao la kusawazisha kipindi cha pili. Barcelona ilishinda mchezo huo kwa magoli 2-1, na Eto’o alishinda tuzo ya mshambuliaji bora baada ya mafanikio yake kwenye kampeni ya Kombe la UEFA. [10][11] Eto'o pia alishinda tuzo ya kihistoria ya tatu mfululizo ya Mchezaji bora wa Afrika msimu huo. Katika hotuba yake ya ushindi, alisema, "Zaidi ya yote, naitoa hii kwa watoto wote wa Afrika." [12] Alichaguliwa pia kwa mara ya pili kwenye kikosi cha kwanza cha dunia cha FIFPro na alishika nafasi ya tatu kwenye kinyang'anyiro cha mchezaji bora wa mwaka chini ya FIFA na kuweka rekodi ya kuwa mchezaji wa pili kutokea Afrika baada ya George Weah kufikia hatua ya tatu bora kwenye tuzo hizo.[13][14]

Msimu uliofuata ulianza vibaya kwa Eto'o baada ya kuumia goti la kulia kwenye mchezo wa hatua ya makundi ya kombe la UEFA dhidi ya SV Werder Bremen mnamo tarehe 27 Septemba 2006. Daktari wa Barcelona Ricard Pruna alitanabaisha kwamba Eto’o angekuwa nje ya uwanja kwa kipindi cha miezi miwili hadi mitatu. [15] Baada ya kufaniwa operation, kipindi cha kukaa nje ya uwanja kiliongezwa mpaka miezi mitano, laini alirudi mazoezini mwanzoni mwa mwezi Januari 2007. [16][17]

2007–09: Tuzo zaidi, Treble na kuondoka

hariri
 
Eto'o wakati wa Kombe la Joan Gamper Trophy mwaka 2008

Eto'o alikataa kuingia kama mchezaji wa akiba kwenye mechi ya ligi dhidi ya Racing de Santander tarehe 11 Februari 2007. Baada ya mchezo huo, meneja wa Barcelona Frank Rijkaard alinukuliwa akisema, "Hakutaka kuingia; sijui kwa nini." [18] Ronaldinho alimkosoa Eto'o kwa kitendo chake, akisema kuwa Eto'o hakuwa anatanguliza maslahi ya timu, lakini Eto'o alikanusha kauli hiyo, akidai kuwa hakutaka kuingia kwa sababu hakuwa amejiandaa vya kutosha kwa mazoezi ya kuingia. [19][20] Miezi mitatu baadaye, Eto'o alisema, "Mambo kama haya kwa kawaida ni uvumi tu na hayasikiki kwangu. Hata hivyo, ikiwa ni kweli kwamba mimi ni tatizo kwa timu yangu basi nitaondoka. Lakini kama nilivyosema, nina furaha hapa. Waandishi wa habari wanaweza kuandika wanachotaka." Kufuatia kauli hizo, Rais wa Barcelona Joan Laporta alikataa uvumi kuhusu uhamisho wa Eto'o na Ronaldinho. [21] Baada ya kuumia tarehe 28 Agosti katika mechi ya kirafiki wakati wa majira ya joto dhidi ya Inter Milan, Eto'o aliondolewa kwenye kikosi kwa muda usiojulikana. [22] Tarehe 17 Oktoba, wakati wa kipindi cha kujiuguza, alipata uraia wa Uhispania. [23] Aliidhinishwa kucheza tena tarehe 4 Desemba na kurejea uwanjani wiki moja baadaye kwenye ushindi wa Barcelona wa 2–1 dhidi ya Deportivo de La Coruña. [24][25] Pep Guardiola aliteuliwa kuwa meneja mpya wa Barcelona kwa msimu wa 2008–09. Kocha huyo alizua gumzo kwa kutangaza kwamba nyota kama Ronaldinho, Deco, na Eto'o hawakuwa sehemu ya mipango yake; hatimaye Eto'o alibaki kwenye klabu, huku wenzake wakiondoka, ingawa kulikuwa na ripoti za kutoelewana kati ya Eto'o na Guardiola. [26][27] Eto'o alipata hat-trick yake ya kwanza ya ligi kwenye mechi dhidi ya Levante tarehe 24 Februari 2008. [28] Alimaliza msimu akiwa na jumla ya mabao 16 katika mechi 18 za ligi. [29]

 
Eto'o akiwa mbele ya Patrice Evra wa Manchester United kwenye fainali za UEFA mwaka 2009

Mnamo tarehe 25 Oktoba, Eto'o aliweka rekodi ya hat-trick ya haraka zaidi katika historia ya ngazi ya klabu baada ya kufunga mara tatu ndani ya dakika 23 katika ushindi dhidi ya Almería.[30] Mechi mbili tu baadaye, mnamo tarehe 8 Novemba 2008, Eto'o alifunga mabao manne katika kipindi cha kwanza kwenye mchezo wa Barcelona dhidi ya Real Valladolid, ambayo ilimalizika kwa ushindi wa 6–0. Mnamo tarehe 29 Novemba 2008, alifunga bao lake la 111 akiwa na Barcelona katika mashindano yote kwenye ushindi wa ugenini wa 3–0 dhidi ya Sevilla, hatua ambayo ilimfanya kuingia katika orodha ya wachezaji kumi bora ya wafungaji wa muda wote wa klabu hiyo.[31] Mnamo tarehe 14 Februari 2009, alifunga bao lake la 99 na la 100 katika mechi za ligi akiwa na Barcelona kwenye sare ya 2–2 dhidi ya Real Betis. Eto'o alifunga bao lake la 30 kwa msimu wa 2008–09 katika mechi ya La Liga dhidi ya Real Valladolid. Mechi hiyo ilimalizika kwa ushindi wa 1–0, ambao ulihakikisha Barcelona inabaki na tofauti ya pointi sita dhidi ya Real Madrid katika ligi. Pia alifunga dhidi ya Villarreal katika mechi ambayo iliwaweka Barcelona hatua moja karibu na kutwaa taji la La Liga 2008–09. Alimaliza msimu akiwa na mabao 30, akishika nafasi ya pili katika orodha ya wafungaji bora nyuma ya mchezaji wa Atlético de Madrid, Diego Forlán. Eto'o alifunga bao la kwanza kwenye mchezo wa fainali ya UEFA yam waka 2009 dhidi ya Manchester United. Barcelona walishinda fainali hiyo kwa magoli 2–0, hivyo kukamilisha Treble. Utatu uliowajumuisha Lionel Messi (mabao 38), Eto'o (mabao 36), na Thierry Henry (mabao 26) walifunga mabao 100 kwa pamoja katika mwaka wa kihistoria wa klabu hiyo.[32]

Inter Milan

hariri

2009–10: Kampeni ya kihistoria ya Treble

hariri
 
Eto’o akichezea Inter Milan mnamo Agosti 2009

Baada ya Maxwell kukamilisha uhamisho kutoka Inter Milan, Joan Laporta alithibitisha kwamba kulikuwa na makubaliano ya pande mbili kati ya Barcelona na Inter Milan ya uhamisho wa Zlatan Ibrahimovic kujiunga na klabu hiyo kwa kubadilishana na Eto'o pamoja na Euro milioni 46.[33][34] Baada ya Ibrahimović kukubaliana masharti na Barcelona, klabu ilitangaza kwamba Eto'o angeenda Milan kwa ajili ya uchunguzi wa afya kukamilisha uhamisho.[35]

Tanbihi

hariri
  1. Kigezo:Cite magazine
  2. "La revancha de Eto'o". Fox Sport. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 28 Oktoba 2010. Iliwekwa mnamo 20 Oktoba 2006.
  3. "QUI SUIS JE ? Samuel, Eto´o Fils". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 9 Novemba 2007.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  4. El Mundo. Mallorca shatters Bernabéu
  5. El País. Mallorca finishes Madrid
  6. McCoy, Tim. "Six to watch in the Primera Liga", BBC Sport, 26 August 2004. 
  7. "Eto'o is Barça priority", BBC Sport, 12 July 2004. 
  8. "Eto'o apologizes for outburst", BBC Sport, 15 May 2005. 
  9. "Eto'o aims for even better at Barça", UEFA, 29 June 2005. 
  10. "Ronaldinho delivers for Barcelona". UEFA. 1 Juni 2006. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 15 Septemba 2008. Iliwekwa mnamo 26 Novemba 2008.
  11. Haslam, Andrew (24 Agosti 2006). "Ronaldinho reigns in Monaco". UEFA. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 8 Desemba 2008. Iliwekwa mnamo 26 Novemba 2008.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  12. "Eto'o king of Africa once again Eto'o show", BBC Sport, 16 February 2006. 
  13. "Ronaldinho voted FIFPro World Player of the Year again". FIFPro. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 21 Desemba 2008. Iliwekwa mnamo 26 Novemba 2008.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  14. "FIFA World Player". FIFA. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 28 Mei 2010. Iliwekwa mnamo 26 Novemba 2008.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  15. "Eto'o setback for Barcelona", The Guardian, 29 September 2006. 
  16. "Eto'o out for five months after knee operation". ESPN. 27 Septemba 2006. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 9 Desemba 2008. Iliwekwa mnamo 26 Novemba 2008.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  17. "Eto'o to train again on Monday", BBC Sport, 11 January 2007. 
  18. Chick, Alex (17 Februari 2007). "Eto'o refuses to play". Eurosport. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 9 Januari 2016. Iliwekwa mnamo 17 Februari 2007.
  19. "Cameroon: Ronaldinho Slams Eto'o – Over Racing snub". allAfrica.com. 17 Februari 2007. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 16 Februari 2007. Iliwekwa mnamo 17 Februari 2007.
  20. "Eto'o slams Rijkaard and Ronaldinho". Eurosport. 14 Februari 2007. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 16 Februari 2007. Iliwekwa mnamo 14 Februari 2007.
  21. "No Change at Barca, Says Chairman". Agence France-Presse. 19 Juni 2007. Iliwekwa mnamo 26 Novemba 2008.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  22. "Eto'o cleared to return to action", BBC Sport, 4 December 2007. 
  23. "Eto'o nationalized" (kwa Kihispania). FC Barcelona. 17 Oktoba 2007. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 22 Januari 2013. Iliwekwa mnamo 26 Novemba 2008.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  24. Jensen, Pete. "Barcelona 2 Deportivo la Coruna 1: Barcelona achieve harmony with REM's return to stage", The Independent, 10 December 2007. 
  25. "Lyon and Fenerbahce roll on". UEFA. 12 Desemba 2007. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 7 Desemba 2008. Iliwekwa mnamo 26 Novemba 2008.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  26. Taylor, Daniel. "Barcelona clear way for Deco, Ronaldinho and Eto'o to leave", 18 June 2008. 
  27. "Eto'o blasts 'coward' Guardiola". ESPN.com. 24 Machi 2014. Iliwekwa mnamo 11 Machi 2024.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  28. Jensen, Pete. "Eto'o hat-trick keeps Barcelona in hot pursuit", The Independent, 25 February 2008. 
  29. Barclay, Patrick. "Eto'o out to prove class is permanent", The Irish Independent, 7 July 2008. 
  30. Jensen, Pete. "Eto'o treble maintains Barcelona's flying start", The Independent, 27 October 2008. 
  31. "Eto'o is one of Barça's top ten all-time goalscorers". fcbarcelona.cat. 30 Novemba 2008. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 30 Julai 2012. Iliwekwa mnamo 1 Desemba 2008.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  32. "Lionel Messi Excelled In The Least Successful Barcelona Under Guardiola" Archived 26 Agosti 2014 at the Wayback Machine. ESPN. Retrieved 24 August 2014
  33. "Laporta announces agreement in principle with Inter", FC Barcelona, 17 July 2009. Retrieved on 2024-11-25. Archived from the original on 2012-05-26. 
  34. "Ibrahimovic firma por cinco años", FC Barcelona, 27 July 2009. (es) 
  35. "Ibrahimovic will arrive on Sunday", FC Barcelona, 24 July 2009. 
  Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Samuel Eto'o kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.