Zaynab Himid Mohammed
Zaynab Himid Mohammed (Forodhani, mtaa wa Malindi, mjini Zanzibar, 12 Februari 1918 - 31 Desemba 2002) ni miongoni wa wasichana wachache waliobahatika kupata elimu katika kipindi hicho huku msukumo mkubwa wa kusoma ukiwa umetoka kwa baba yake ambaye alikuwa amesafiri sehemu nyingi na kujua umuhimu wa elimu [1].
Zaynab Himid Mohammed | |
Amezaliwa | 12 Februari 1918 Zanzibar |
---|---|
Amekufa | 31 Desemba 2002 Zanzibar |
Nchi | Tanzania |
Majina mengine | Zaynab Himid Mohammed |
Kazi yake | Taaluma ya Kiswahili |
Katika zama za Zaynabu Himid Mohammed hali ya ubaguzi katika elimu katika kisiwa cha Zanzibar ilikuwa imetawala sana na hivyo wazazi wake waliamua kubadili jina katika cheti cha kuzaliwa ili aonekane na jina la Kiarabu na aweze kwenda shule.
Katika miezi ya mwanzo ya Bi Zaynabu kwenda shule alikutana na changamoto nyingi ikiwemo za kurushiwa mawe kwani watu waliamini kuwa elimu haina manufaa yoyote kwa mtoto wa kike.
Zaynabu Himid alianza kupata uzoefu zaidi wa kuandika akiwa shuleni kama mwalimu ambapo alikuwa akiandika michezo ya kuigiza na hotuba.
Muda mfupi baada ya Mapinduzi ya Zanzibar rais wa kwanza wa Zanzibar Abeid Amani Karume alimpa kazi ya kuandika mchezo wa kuigiza ulioitwa Unguja ya leo si ya jana, mchezo ambao ulikuja kuonyeshwa mbele ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Mbali na kuandika mchezo huo, pia aliwahi kuitwa na waziri mmoja na kupewa kazi ya kuandika shairi kumuhusu Julius Nyerere na shairi hilo liliitwa "Nyerere raisi mwema mwenye busara na hima".
Zaynab Himid Mohammed alifariki dunia akiwa na umri wa miaka themanini na nne.
Tanbihi
hariri- ↑ Mohammed, Zaynab Himid. (2004). Howani mwana Howani : tenzi za Zaynab Himid Mohammed. Dar es Salaam: Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. ISBN 9776911645. OCLC 144607717.
{{cite book}}
: Check|isbn=
value: checksum (help)
Makala hii kuhusu mwandishi fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Zaynab Himid Mohammed kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |