Zeland
(Elekezwa kutoka Zealand)
Zeland (kwa Kidenmark: Sjælland) ni kisiwa kikubwa cha Denmark kilichopo kwenye mashariki ya nchi hiyo. Inatenganishwa na Uswidi kwa mlangobahari wa Øresund upande wa mashariki. Eneo la Zeland ni kilomita za mraba 7,031.
Kuna wakazi wapatao 2,268,000 wanaoishi kisiwani kufuatana na sensa ya mwaka 2016. Wengi wao wanaishi karibu na Kopenhagen ambayo ni mji mkuu wa Denmark.
Zeland imeunganishwa na sehemu nyingine za Denmark kwa njia ya madaraja na njia chini ya bahari ambayo ni pamoja na:
- Daraja la Belt Kubwa ambalo linaunganisha Zeland na Funen, kisiwa cha magharibi.
- Daraja la Storstrøm, linalounganisha Zeland na Lolland, kisiwa cha kusini.
- Daraja la Øresund, ambalo linaunganisha Zeland na Uswidi upande wa mashariki, karibu na Malmö.
Makala hii kuhusu maeneo ya Ulaya bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Zeland kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |