Ziwa Kitangiri
Ziwa Kitangiri ni kati ya maziwa madogo ya Tanzania.
Linapatikana katika mkoa wa Singida, wilaya ya Iramba, tarafa za Shelui na Kisiriri. Shughuli zifanywazo katika ziwa hili ni uvuvi wa samaki wa aina mbalimbali kama vile: kambale, kamongo, perege, nembe na ningu. Ziwa Kitangiri limekuwa chanzo kikubwa cha uchumi katika wilaya ya Iramba.
Kuna wanyama wengine waishio humo kama vile kiboko n.k.
Pia kuna ndege wengi wa aina mbalimbali wazuri wa kuvutia; ndege hao ni: flamingo, korongo, ndegemwambu (bwana usafi), fongafonga, batamaji, batamzinga n.k.
Tazama pia
haririTanbihi
haririViungo vya nje
haririMakala hii kuhusu maeneo ya Tanzania bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Ziwa Kitangiri kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. Usitaje majina ya madiwani na viongozi au maafisa wengine wa sasa maana wanabadilika haraka mno. |