Wilaya ya Iramba ni wilaya mojawapo kati ya 7 za Mkoa wa Singida.

Mahali pa Iramba (kijani cheusi) katika mkoa wa Singida.

Imepakana na Mkoa wa Shinyanga upande wa kaskazini-Magharibi, na Mkoa wa Mara upande wa kaskazini-mashariki, wilaya ya Singida Vijijini na Singida Mjini upande wa kusini na Mkoa wa Tabora upande wa magharibi

Katika sensa ya mwaka 2002, idadi ya wakazi wa wilaya hiyo ilihesabiwa kuwa 236,282.[1] Katika sensa ya mwaka 2022 walihesabiwa 328,912 [2].

Sehemu kubwa ya wenyeji wa Iramba ni Wanyiramba wanaosema lugha ya Kinyiramba.

Marejeo hariri

  Kata za Wilaya ya Iramba - Mkoa wa Singida - Tanzania  

Kaselya | Kidaru | Kinampanda | Kiomboi | Kisiriri | Kyengege | Maluga | Mbelekese | Mgongo | Mtekente | Mtoa | Mukulu | Ndago | Ndulungu | Ntwike | Old-Kiomboi | Shelui | Tulya | Ulemo | Urughu


  Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Singida bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Iramba kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Usitaje majina ya madiwani na viongozi au maafisa wengine wa sasa maana wanabadilika haraka mno.