Zotiko wa Konstantinopoli
Zotiko wa Konstantinopoli (labda Roma, Italia, karne ya 4 - Konstantinopoli, katika Uturuki wa leo, 350) alikuwa padri aliyesemekana kuwa alimfuata Konstantino Mkuu katika mji wake mpya ili kumsaidia kuuanzisha.
Huko kwa miaka ishirini alishughulikia mayatima na maskini na kuwajengea hospitali kama ilivyoagizwa na Mtaguso wa kwanza wa Nisea[1].
Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu, pengine mfiadini.
Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 31 Desemba[2].
Tazama pia
haririTanbihi
haririMakala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |