Dolar ya Marekani

(Elekezwa kutoka $)

Dolar ya Marekani (pia: dola, US-Dollar, kifupi USD) ni pesa halali ya Marekani. Alama yake ni $.

Noti za Dola ya Marekani.

Dolar ya Marekani inapatikana kwa noti za dola 1, 2, 5, 10, 20, 50 na 100. Kuna pia sarafu ya dola 1.

Dolar moja ina senti 100. Senti huitwa pia "penny" nchini Marekani. Kuna sarafu za nusu dolar (half dollar, senti 50), robo dolar (quarter, senti 25) na sarafu za senti 10 (dime), 5 (nickel) na 1 (penny).

Hadi mwaka 1969 noti ya dolar ya Marekani ilikuwa na ahadi ya kwamba serikali ya Marekani itampatia kila mtu dhahabu kulingana na thamani ya dola hizi akipenda kuzibadilisha.

Usawa huu na thamani ya dhahabu ulifutwa. Leo hii dolar ya Marekani ni pesa ya kuiamini serikali kama pesa zote. Maana yake watumiaji husadiki ya kwamba serikali haitachapisha dola kushinda uwezo wa uchumi na thamani ya bidhaa zilizopo nchini Tanzania.

Tangu mwisho wa Vita Kuu ya Pili ya Dunia (1945) dolar ya Marekani imekuwa pesa kuu duniani na sehemu kubwa ya biashara ya kimataifa hukadiriwa kwa dolar hizo. Lakini tangu kupatikana kwa Euro mwaka 1999 umuhimu wa dolar ya Marekani imeanza kupungua polepole. Hata hivyo nchi mbalimbali zimeachana na sarafu zao na kuamua kutumia dolar ya Marekani tu, k.mf. El Salvador.

Viungo vya nje

hariri
 
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
  Makala hii kuhusu mambo ya uchumi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Dolar ya Marekani kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.