Aaliyah Dana Haughton (16 Januari 197925 Agosti 2001) alikuwa msanii wa rekodi, mwigizaji, na mwanamitindo kutoka nchini Marekani. Alijulikana sana kwa jina la kisanii kama Aaliyah. Aaliyah alizaliwa mjini Brooklyn, New York, na kukulia mjini Detroit, Michigan. Wakati wa umri wake wa awali, amepata kuonekana kwenye kipindi cha televisheni cha Star Search na kutumbuiza kwenye onyesho hilo na Gladys Knight. Akiwa na umri wa miaka 12, Aaliyah aliingia mkataba na Jive Records na Blackground Records na mjomba wake, Barry Hankerson. Akamtambulisha kwa R. Kelly, ambaye baadaye akaja kuwa mshauri wake, vilevile mtunzi na mtayarishaji wake kiongozi wa albamu yake ya kwanza, Age Ain't Nothing But a Number. Albamu iliweza kuuza nakala milioni mbili kwa nchini Marekani na kutunukiwa platinamu mbili na Recording Industry Association of America (RIAA). Baada ya kukumbwa na mshtaka ya ndoa haramu na Kelly, Aaliyah akavunja mkataba wake na Jive na badala yake kuingia mkataba na studio ya Atlantic Records.

Aaliyah
Aaliyah mnamo mwaka 2000.
Aaliyah mnamo mwaka 2000.
Maelezo ya awali
Jina la kuzaliwa Aaliyah Dana Haughton
Amezaliwa (1979-01-16)Januari 16, 1979
Brooklyn, New York City, New York, United States
Asili yake Detroit, Michigan, United States
Amekufa Agosti 25, 2001 (umri 22)
Marsh Harbour, Visiwa vya Abaco, The Bahamas
Aina ya muziki R&B, pop, hip hop
Kazi yake Mwimbaji, mnenguaji, mwigizaji, mwanamitindo
Miaka ya kazi 1991–2001
Studio Blackground, Jive, Atlantic, Virgin, Universal
Tovuti www.aaliyah.com

Aaliyah amefanya kazi na watayarishaji kama vile Timbaland na Missy Elliott kwa ajili ya albamu yake ya pili ya One in a Million; imeuza nakala milioni mbili kwa nchini Marekani na nakala zaidi ya milioni nane kwa hesabu ya dunia nzima. Mnamo mwaka wa 2000, Aaliyah amepata kuonekana kwenye filamu yake ya kwanza -liokwenda kwa jina la Romeo Must Die. Amechangia kibwagizo cha filamu hiyo, ambacho ni "Try Again". Wimbo ulishika nafasi ya juu kwenye chati za Billboard Hot 100 katika airplay pekee, inamfanya Aaliyah kuwa msanii wa kwanza kufaula hivi katika historia ya Billboard. "Try Again" imepata kushindinishwa kwenye Grammy Award kwa ajili Msanii Bora wa Kike wa R&B.

Diskografia hariri

Albamu za Studio hariri

Kompilesheni hariri

Tanbihi hariri

Marejeo hariri

Viungo vya Nje hariri

  Makala hii kuhusu mwanamuziki/wanamuziki fulani wa Marekani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Aaliyah kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.