Actors Studio
40°45′36″N 73°59′34″W / 40.760068°N 73.992654°W
Actors Studio ni shirika la uwanachama kwa ajili ya waigizaji wa kulipwa, waongozaji wa tamthilia na waandishi wake katika 432 West 44th Street mjini Clinton karibia na Manhattan huko New York City. Shirika lilianzishwa mnamo tar. 5 Oktoba 1947, na Elia Kazan, Cheryl Crawford, Robert Lewis na Anna Sokolow ambaye ndiye aliyefundisha harakati za waigizaji kuwa wanachama.[1] Lee Strasberg alijunga baadaye na kuchukua uongozi mnamo 1951 hadi kifo chake kunako 17 Februari 1982. Kwa sasa shirika linaendeshwa na Al Pacino na Ellen Burstyn. Studio hii ni mashahuri sana kwa kazi zake za kuboresha na kufundisha namna ya kuigiza. Wazo hili lilitokana na Group Theatre kunako miaka ya 1930 kulingana na uvumbuzi wa Constantin Stanislavski. Wakati katika Studio, waigizaji wanafanya kazi pamoja ili kukuza maarifa yao katika hali ya kujitegemea, ambapo wanaweza wakachukua hatua kama waigizaji bila kupata msukumo wowote wa kujihusisha na masuala ya kibiashara.
Kundi hili walikuwa wakifanyia mazoezi yao katika sehemu ya Princess Theatre [2] Mwaka wa 1955 wakahamia katika sehemu yao ya sasa ambapo zamani kulikuwa eneo la kanisa la Wasabato, -mejengwa mnamo 1859.[3]
Mwaka wa 1965 Actors Studio wamefungua tawi lao huko katika pwani ya magharibi mjini West Hollywood, California. The Actors Studio West inaendeshwa na uongozi wa kisanii-kiongozi ambapo kuna Mark Rydell na Martin Landau na ni tawi rasmi pekee la Actors Studio duniani.
Muundo
haririRais[4]
- Paul Newman (1982–1994)
- Al Pacino (1994–hadi sasa)
- Ellen Burstyn (1994–hadi sasa)
- Harvey Keitel (1994–hadi sasa)
Viongozi Wasanii (New York):[4]
- Lee Strasberg (1951–1982)
- Al Pacino (1982)
- Ellen Burstyn (1982–1988)
- Frank Corsaro (1988–1995)
- Arthur Penn (1995–1998)
- Estelle Parsons (1998–2003)
- Vacant (2003–2004)
- Stephen Lang (2004–2006)
- Carlin Glynn (2004–2007)
- Lee Grant (2004–2007)
- Ellen Burstyn (2007–hadi sasa)
Wahitimu maarufu
haririKulingana na historia yake ndefu ya kutoa waigizaji mashuhuri na wenye mafanikio, waongozaji na waandishi waliotokana na studio, ni pamoja na:[5][6]
Soma zaidi
hariri- A Method to their Madness: The History of the Actors Studio, by Foster Hirsch. Da Capo Press, 1986. ISBN 0306802686.
- The Actors Studio: a History, by Shelly Frome. McFarland, 2001. ISBN 0786410736. cassandra morency
Marejeo
hariri- ↑ Anna Sokolow The Rebelious Spirit by Larry Warren page 89 – 94 :The Actors Studio ISBN 90-5702-185-4
- ↑ in Focus by S. Carnicke – Routledge; (1 Novemba 1998) ISBN 9057550709
- ↑ From Abyssinian to Zion: A Guide to Manhattan's Houses of Worship by David W. Dunlap – Columbia University Press (21 Aprili 2004) ISBN 0231125429
- ↑ 4.0 4.1 "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2011-10-21. Iliwekwa mnamo 2011-11-03.
- ↑ Lipton, James. Inside Inside, Dutton, (2007) p. 14, other names listed
- ↑ "Pace University Actors Studio MFA". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2010-06-18. Iliwekwa mnamo 2011-11-03.
Viungo vya Nje
hariri- The official web site of the Actors Studio
- PBS American Masters Series profile
- Inside the Actors Studio Ilihifadhiwa 18 Aprili 2003 kwenye Wayback Machine.
- The Actors Studio MFA Program at Pace University Ilihifadhiwa 23 Desemba 2007 kwenye Wayback Machine.
- Audio collection of the Actors Studio from 1956–69 at the Wisconsin Historical Society
Makala hii kuhusu mambo ya elimu bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Actors Studio kama historia yake, uenezi au maendeleo yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |