Adalbert wa Magdeburg

Mtakatifu Adalbert wa Magdeburg

Mtakatifu Adalbert wa Magdeburg (na Adalbert wa Magdeburg) (alifariki tarehe 20 Juni, 981) alikuwa mmisionari na askofu mkuu wa kwanza wa mji wa Magdeburg, Ujerumani.

Ametambuliwa kuwa mtakatifu.

Sikukuu yake ni tarehe 20 Juni.

MaishaEdit

Adalbert alizaliwa Ujerumani na kuwa mtawa katika monasteri ya Wabenedikto wa mji wa Trier.

Baada ya kuwekwa wakfu kama askofu, mwaka 961 alitumwa mjini Kiev (Ukraine) kama mmisionari.

Kundi lake lote liliuawa, naye peke yake aliweza kurudi Ujerumani.

Baadaye aliteuliwa kuwa askofu mkuu wa dayosisi ya Magdeburg.

Alianzisha madayosisi mapya mengi upande wa Mashariki wa Ujerumani, kama katika miji ya Naumburg, Meisen, Merseburg, Brandenburg, Havelberg, na Poznan.

Mwanafunzi wake mmoja aliyetangazwa kuwa mtakatifu kama yeye ni Adalbert wa Praha.

Tazama piaEdit

MarejeoEdit

Viungo vya njeEdit

  Makala hii kuhusu Mkristo huyu bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Adalbert wa Magdeburg kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.