Agrisi wa Trier (kwa Kilatini: Agricius au Agritius; 260 hivi[1] - Trier, leo nchini Ujerumani, 329/335) alikuwa askofu wa kwanza kujulikana kwa hakika wa mji huo kwa kuwa alishiriki Mtaguso wa Arles mwaka 314[2].

Mt. Agrisi.

Aligeuza ikulu, iliyotolewa na malkia Helena, kuwa kanisa.

Tangu kale anaheshimiwa na Kanisa Katoliki na Kanisa la Kiorthodoksi kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 13 Januari[3] au 19 Januari.

Tazama pia hariri

Tanbihi hariri

  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.