Ahmed Sékou Touré

Ahmed Sékou Touré (au Ahmed Sheku Turay; 9 Januari 1922 - 26 Machi 1984) alikuwa kiongozi wa kisiasa; mkuu wa PDG kutoka nchini Guinea.

Sekou Toure.

Alichaguliwa kama Rais wa kwanza wa Guinea akatumikia kuanzia mwaka 1958 hadi kifo chake 1984. Touré alikuwa miongoni mwa wazalendo wa awali wa Guinea waliojishughulisha katika harakati za kupigania uhuru wa nchi kutoka mikononi mwa Wafaransa.

Mwaka wa 1960, alitangaza chama chake cha Parti démocratique de Guinée (PDG) kuwa chama halali pekee nchini humo na kuongoza tangu hapo kwa utawala wa kiimla. Alichaguliwa kwa maneno tu kwa vipindi saba vya miaka saba, lakini Guinea haikuwa na chama kingine cha kisiasa, na aliwafunga au kuwafukuza nchini viongozi wakubwa wa upinzani dhidi yake .

Alikuwa kitukuu wa Samori Ture, mwanzilishi wa Dola la Wasulu.

Mnamo Oktoba 2021, kwenye hafla ya maadhimisho ya miaka 50 ya mauaji ya Oktoba 1971, jamaa za watu 70 wa Guinea walioangamizwa chini ya utawala wa Sekou Touré walimwomba Rais Mamady Doumbouya ukarabati na mazishi ya heshima kwa waathiriwa.

Marejeo

hariri
  • Henry Louis Gates, Anthony Appiah (eds). Africana: The Encyclopedia of the African and African, "Ahmed Sékou Touré," pp1857–58. Basic Civitas Books (1999). ISBN 0-465-00071-1
  • Molefi K. Asante, Ama Mazama. Encyclopedia of Black Studies. Sage Publications (2005) ISBN 0-7619-2762-X
  • (Kifaransa) Ibrahima Baba Kake. Sékou Touré. Le Héros et le Tyran. Paris, 1987, JA Presses. Collection Jeune Afrique Livres. 254 p
  • Lansiné Kaba. "From Colonialism to Autocracy: Guinea under Sékou Touré, 1957–1984;" in Decolonization and African Independence, the Transfers of Power, 1960-1980. Prosser Gifford and William Roger Louis (eds). New Haven: Yale University Press, 1988.
  • Phineas Malinga. "Ahmed Sékou Touré: An African Tragedy" Archived 22 Oktoba 2018 at the Wayback Machine.
  • Baruch Hirson. "The Misdirection of C.L.R. James", Communalism and Socialism in Africa, 1989.
  • John Leslie. Towards an African socialism, International Socialism (1st series), No.1, Spring 1960, pp. 15–19.
  • (Kifaransa) Alpha Mohamed Sow, "Conflits ethnique dans un État révolutionnaire (Le cas Guinéen)", in Les ethnies ont une histoire, Jean-Pierre Chrétien, Gérard Prunier (ed), pp. 386–405, KARTHALA Editions (2003) ISBN 2-84586-389-6
  • Parts of this article were translated from French Wikipedia's fr:Ahmed Sékou Touré.

Viungo vya Nje

hariri
  Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Ahmed Sékou Touré kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.