Aleksanda wa Makaa

Aleksanda wa Makaa (alifariki Gumenek, leo nchini Uturuki, 251 hivi) alikuwa askofu wa mji huo maarufu kwa unyenyekevu wake uliomfanya apende kudharauliwa. Njia mojawapo ilikuwa kufanya kazi ya kuchoma makaa na kuwa mchafu [1].

Kwa njia ya falsafa alikuwa amefikia utambuzi wa pekee wa unyenyekevu wa Kikristo; ndipo Gregori Mtendamiujiza alipomuinua kuongoza Kanisa hilo, alipong'aa kwa mahubiri yake na hatimaye kwa kuchomwa moto kwa ajili ya imani yake wakati wa dhuluma ya kaisari Decius[1].

Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu mfiadini.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 11 Agosti[2].

Tazama pia

hariri

Tanbihi

hariri

Viungo vya nje

hariri
  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.