Milima ya Altai
(Elekezwa kutoka Altai Mountains)
Milima ya Altai ni safu ya milima katika Asia ya Kati na ya Mashariki. Milima mirefu zadi hufikia kimo cha mita 4,500.
Urusi, China, Mongolia, na Kazakhstan zinakutana katika milima hii, ambayo ni chanzo cha mito ya Irtysh na Ob.
Safu hiyo imeungwa na Milima ya Sayan kwenye kaskazini mashariki ikiishia upande wa kusini mashariki katika Jangwa la Gobi.
Wakazi wa eneo lake si wengi wakiwa mchanganyiko wa Warusi, Wakazakhi, Waaltai na Wamongolia.
Uchumi wa eneo hilo unategemea ufugaji wa ng'ombe, farasi na kondoo, pamoja na kilimo, misitu, na uchimbaji madini.
Sehemu ya safu hiyo imeorodheshwa na UNESCO kama urithi wa dunia.
Viungo vya nje
hariri- "Ancient spirit and might preserved by indigenous people of Altay." katika YouTube RT . 6 Novemba 2011.
- Mwongozo wa Mlima Altai Ilihifadhiwa 2 Desemba 2019 kwenye Wayback Machine. - Karibu Altai
- Picha za Mlima Altai - Altai-Picha
- Milima ya Dhahabu ya Altai katika Mfuko wa Ulinzi wa Urithi wa Maliasili
- Tathmini ya UNESCO ya Altai (faili la PDF)
Makala hii kuhusu maeneo ya Asia bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Milima ya Altai kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |