Amandina Lihamba

Mwigizaji

Amandina Lihamba (alizaliwa mwaka 1944) ni mwigizaji na muongozaji wa filamu kutoka Tanzania. Ni profesa wa chuo kikuu cha Dar es Salaam katika kitengo cha Sanaa. Amewahi kuwa mshauri wa wanafunzi chuoni hapo, mkuu wa idara na mjumbe wa bodi chuoni hapo.

Mnamo mwaka 1989 alikuwa mmoja wa waanzilishi wa mradi wa Jukwaa la Watoto. Pia ni mwanzilishi wa kundi la wasichana la kuigiza (drama) katika mchezo ujulikanao kama Tuseme akishirikiana na Penina Muhando mnamo mwaka 1998.[1]

Lihamba alizaliwa katika wilaya ya Morogoro mnamo mwaka 1944.[2].Alipata shahada ya uzamivu kutoka chuo kkikuu cha Leeds(University of Leeds).

Katika masomo yake ya uzamivu (udaktari) alijikita katika masuala ya Siasa na Sanaa nchini Tanzania baada ya Azimio la Arusha miaka 1967-1984.[3]

Katika uzamivu huo, anaelezea ni kwa namna gani neno ngonjera lilijitokeza kama propaganda za chama tawala kwa namna isivyotakiwa.[4]

Lihamba alifuata mfano wa muongoza filamu kutoka Senegal aitwaye Ousmane Sembène aliyeongoza filamu ya The Money-Order [5] iliyotoka mwaka 1968 ambayo pia hujulikana kwa jina la Mandabi

Filamu hariri

  • The Marriage of Mariamu (1985)
  • Khalfan and Zanzibar (1999)
  • Maangamizi: The Ancient One (2001)

Marejeo hariri

  1. Koch, Jule (2008). Karibuni Wananchi: Theatre for Development in Tanzania : Variations and Tendencies. Eckersdorf [Germany]: Thielmann & Breitinger. uk. 107. ISBN 978-3-939661-06-1. 
  2. Akyeampong, Emmanuel K.; Gates, Jr., Henry Louis, wahariri (2012). "Lihamba, Amandina (1944– )". Dictionary of African Biography. Oxford: Oxford University Press. ISBN 978-0-19-538207-5. 
  3. Plastow, Jane (1996). African Theatre and Politics: The Evolution of Theatre in Ethiopia, Tanzania and Zimbabwe: A Comparative Study. Amsterdam [u.a.]: Rodopi. uk. 3. ISBN 978-90-420-0038-4. 
  4. Justice-Malloy, Rhona, mhariri (2010). Theatre History Studies 2010 (toleo la 2nd). Tuscaloosa: University of Alabama Press. ku. 35, 40. ISBN 978-0-8173-7107-4. 
  5. Mwangi, E. (2009). "Amandina Lihamba's gendered adaptation of Sembene Ousmane's The Money-Order". Research in African Literatures 40 (3): 149–173. doi:10.2979/ral.2009.40.3.149. 
  Makala hii kuhusu mwigizaji filamu fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Amandina Lihamba kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.