Amasio wa Teano (alifariki 356 hivi) alikuwa askofu wa pili wa mji huo, leo nchini Italia, kuanzia mwaka 346 hadi kifo chake.

Inasemekana alitokea Ugiriki akiwa padri baada ya kufukuzwa na kaisari Constantius II kwa kukataa mafundisho ya Ario[1].

Papa Julius I alimtuma Campania ambapo Wakatoliki wa Teano walimpokea kama askofu wao[2].

Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu[3].

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 23 Januari[4].

Tazama pia

hariri

Tanbihi

hariri
  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.