Amelia Kajumulo Kivaisi
Amelia Kajumulo Kivaisi ni profesa mstaafu wa mikrobiolojia tumizi. Alikuwa mwanachama mwanzilishi na mkuu wa kwanza wa Idara ya biolojia ya molekuli (MBB) katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) ambapo amekua profesa kwa takriban miaka 15. Kwa sasa anafanya kazi kwa mkataba katika idara hiyohiyo.[1].
Amelia Kajumulo Kivaisi | |
---|---|
Utaifa | Mtanzania |
Majina mengine | Profesa Amelia |
Kazi yake | Mkufunzi wa chuo kikuu cha Dar es Salaam, Mjasiliamali, Mtafiti |
Hivi karibuni ametunukiwa cheo cha profesa "emerita", akiwa kwenye jopo la kwanza la wanataaluma na mwanamke wa kwanza kutunukiwa cheo hicho kutoka chuo kikuu cha Dar es Salaam [2].
Elimu
haririAmelia ni msomi ambaye ana elimu za shahada ya pili (MSc) na shahada ya uzamivu (PhD) ya sayansi ya mikrobiolojia na alijikita katika mmeng'enyo anaerobia wa mabaki ya kilimo ya lignicellulosic.
Kazi
haririAmelia amekuwa mtafiti kwa miaka mingi, utafiti wake ulilenga ubadilishaji wa kibiolojia wa taka ngumu za kikaboni kuwa gesi ya asilia, uyoga na viuatilifu vya kibilojia. Amesimamia na kushauri wanafunzi wengi wa shahada ya pili (MSc) na shahada ya uzamivu (PhD) na kuongoza miradi kadhaa ya kitaifa na ya kimataifa ya utafiti.
Kwa kushirikiana na washirika wa viwandani, kwa sasa anahusika katika kukuza daraja la biashara-viuatilifu vya kibilojia akiwa kama mhariri mkuu wa Jarida la Sayansi la Tanzania na amechapisha katika majarida kadhaa. Alisambaza zaidi matokeo ya utafiti kupitia ushiriki wa dhati katika mikutano mingi ya kisayansi.
Tafiti
haririHii ni orodha ya baadhi ya tafiti na kazi mbalimbali zilizofanywa na Prof. Amelia
- Matumizi ya taka za viwandani za kilimo
- Usalama wa chakula na ujasiliamali [3]
- Mapinduzi yasiyo ya kijani [4]
- Udongo wa kupandia uyoga [5]
- Sekta ya Mkonge ya Tanzania: Uchunguzi na tabia baada ya mavuno ya mkonge kama uchenjuaji wa kibaiolojia [6]
- Uzalishaji wa kimeng'enya cha Oxidative na Hydrolytic kwa njia ya Coprinus cinereus (Schaeff). Majivu kutoka katika masalia ya mkonge yaliyochanganywa na Kinyesi cha ng'ombe[7]
Pia amehusika na kutoa marejeo na hariri katika tafiti nyingine zilizofanyika nje ya Tanzania. [8]
Marejeo
hariri- ↑ https://www.udsm.ac.tz/web/index.php/staff/name/Amelia%20/165
- ↑ https://www.udsm.ac.tz/web/index.php/offices/aca/professors-emeriti
- ↑ Food for thought: Food security and entrepreneurship
- ↑ http://www.mondofungo.it/Non_Green_Revolution.html
- ↑ https://www.yumpu.com/xx/document/read/11387414/nitapata-wapi-udongo-wa-kupandia-uyoga-uyoga-tanzanian-
- ↑ http://connection.ebscohost.com/c/articles/87992048/tanzania-sisal-industry-auditing-characterization-sisal-post-harvest-wastes-as-bio-resource-bio-refining
- ↑ https://europepmc.org/article/MED/26664748?singleResult=true
- ↑ https://scholar.google.com/citations?user=Rrl9cxwAAAAJ&hl=cs
Makala hii kuhusu mwanasayansi fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Amelia Kajumulo Kivaisi kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |