Anania bin Nedebeus
Anania bin Nebedeus (kwa Kiebrania חנניה בן נדבאי) alikuwa kuhani mkuu wa Israeli miaka 47-52 BK.
Kadiri ya kitabu cha Matendo ya Mitume katika Agano Jipya la Biblia ya Kikristo alitaka kumhukumu Mtume Paulo huko Yerusalemu (23:2) lakini liwali alimpeleka Kaisarea (24:1).
Pia Yosefu Flavius, Antiquities xx. 5. 2, alimzungumzia.[1]
Aliondolewa madarakani ili ahukumiwe Roma.
Hatimaye aliuawa na Wayahudi mwaka 66, mwanzoni mwa Vita vya kwanza vya Kiyahudi dhidi ya Warumi.
Makala hii kuhusu mtu wa Biblia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Anania bin Nedebeus kama habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
Tanbihi
hariri- ↑ Pulpit Commentary on Acts 23 http://biblehub.com/commentaries/pulpit/acts/23.htm accessed 18 October 2015