Kuhani mkuu
Kuhani mkuu ni cheo kikuu cha kuhani katika dini zenye ngazi mbalimbali ya ukuhani. Kwenye mahekalu makubwa yenye makuhani wengi, mmoja aliweza kuwa na nafasi ya kiongozi na kuitwa kuhani mkuu.
Katika dini za Sumeri, Babeli na Misri ya Kale walikuwepo pia makuhani wakuu waliokuwa viongozi wa dini kwa ufalme wote. Katika Babeli kulikuwa pia na makuhani wakuu wa kike.
Katika Israeli ya Kale Kuhani Mkuu (kwa Kiebrania כהן גדול kohen gadol) alikuwa kiongozi mkuu pekee wa ibada za dini ya Uyahudi tangu mwanzo wa taifa la Israeli hadi mwaka 70 B.K., hekalu la Yerusalemu lilipobomolewa moja kwa moja.
Ilibidi awe mwanamume aliyezaliwa na baba wa ukoo wa Haruni, kaka yake Musa.
Wakati wa Yesu alikuwa mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Israeli lenye wajumbe 70 chini yake. Chini ya utawala wa Dola la Roma kuhani mkuu wa Yerusalemu alikuwa pia na wajibu wa kisiasa kama kiongozi wa Wayahudi nchini.
Waraka kwa Waebrania katika Agano Jipya unamtambulisha Yesu Kristo mwenyewe kuwa kuhani mkuu wa milele kufuatana na utaratibu wa Melkisedeki, ukisisitiza ubora wake kulingana na makuhani wa Agano la Kale.
Viungo vya nje
hariri- The Mysterious White Garments of Yom Kippur Archived 8 Aprili 2008 at the Wayback Machine.
- Burial artifact inscribed 'Son of High Priest' found near West Bank fence route
Makala hii kuhusu mambo ya dini bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu mada hii kama historia yake au uenezi wake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |