Andrea wa Soveral na wenzake

Andrea wa Soveral (São Vicente, 1572Cunhau, 16 Julai 1645) alikuwa padri wa Brazil wakati wa ukoloni. Awali alijiunga na shirika la Wajesuiti lakini baadaye aliliacha akabaki mwanajimbo.

Maziara ya wafiadini wa Natal.

Aliuawa kikatili na Waprotestanti pamoja na waumini 69 wakati wa kuadhimisha Misa kanisani[1].

Padri mwingine, Ambrosio Fransisko Ferro, na wenzake 27 waliuawa vilevile tarehe 3 Oktoba mwaka uleule.

Papa Yohane Paulo II aliwatangaza wenye heri tarehe 5 Machi 2000, halafu Papa Fransisko aliwatangaza watakatifu tarehe 15 Oktoba 2017.

Sikukuu yao huadhimishwa tarehe 16 Julai[2].

Tazama pia hariri

Tanbihi hariri

Viungo vya nje hariri

  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.