Anga-nje (kwa Kiingereza outer space) ni eneo la ulimwengu. Tofauti na anga ya dunia yetu inayojazwa na angahewa ni yote nje yake. Sehemu kubwa za anga za nje ni nafasi ambayo inakaribia hali yaombwe. Katika tupu hii kuna magimba ya angani kama sayari, nyota, galaksi, nebula na mawingu.

Muunganisho kati ya uso wa Dunia na Anga-nje. Mstari wa Kármán katika urefu wa kilomita 100 (62 mi) umeonyeshwa. Tabaka za anga huvutwa kwa kiwango, wakati vitu ndani yao, kama Kituo cha Anga cha Kimataifa, sio.

Wanasayansi hawaoni ya kwamba nafasi kati ya magimba ya angani ni hali ya ombwe au tupu kabisa lakini kuna kiasi kidogo cha utegili wa hidrojeni pamoja na mnururisho wa sumakuumeme na nyutrino. Katika nadharia ya fizikia kuna pia mata nyeusi na nishati nyeusi ambazo hazikuthibitishwa bado.

Mipaka ya Anga-nje

hariri

Si rahisi kutaja kikamilifu mpaka baina ya angahewa na anga-nje la Dunia. Kuna majaribio mbalimbali kufafanulia mpaka huo. Wengine wanaona inaanza katika kanda la tabakanje ya angahewa. Shirika la Federation Aeronautique Internationale linataja kimo cha kilomita 100 na NASA inataja kimo cha kilomita 80 ambazo ni takriban sawa na mpaka baina tabakakati na tabakajoto. Hata hivyo, satelaiti zinazotumia obiti za karibu hadi km 500 juu ya uso wa ardhi, bado zinaathiriwa na viwango vidogo vya hewa vinavyoenea hadi kimo kile.

Kwa upande mwingine mipaka ya nje ya anga haijulikani kabisa. Nadharia mbalimbali zinadai ama anga za nje halina mwisho, au kuwa anga za nje inaendelea kupanuka ilhali imefikia umbali wa takriban miaka nuru bilioni 13 -14.

Kufuatana na nadharia ya mlipuko mkuu anga lilianza kama nukta likaendelea kupanuka hadi leo na kwa wakati ujao. Kufuatana na nadharia hii umbali kati dunia yetu na nyota inaendelea kuongezeka.

Upelelezi wa Anga-nje

hariri

Utafiti kamili wa anga-nje ni vigumu kutokana na ukubwa wake. Nadharia zote zinategemea vipimo vya nuru na mnururisho zinazofika duniani au karibu nayo. Njia nyingine ni kutuma vyombo vya angani kwenda safari ya anga za nje lakini kutokana na umbali mkubwa mno haziwezi kufika mbali kweli. Chombo cha angani kilishosafiri mbali hadi sasa ni Voyager 1 iliyoondoka duniani mwaka 1977 na hadi sasa imepita sayari za Uranus na Neptuni. Chombo cha New Horizon kiliondoka dunaini mwaka 2006 kiliipita Pluto mwaka 2015 na kuendelea hadi ndani ya kanda la Kuiper.

Hali ya kisheria ya Anga-nje

hariri

Nchi za Umoja wa Mataifa ziliunda mkataba wa kimataifa juu ya anga za nje kwa azimio la mkutano mkuu wa UM mwaka 1963. 1967 Umoja wa Kisovyeti, Marekani na Ufalme wa Maungano (Uingereza) zilitia sahihi mkataba huu kama madola ya kwanza. Hadi 2008 nchi 98 zimeikubali kisheria na nchi 27 za ziada zimetia sahihi.

Katika mkataba huu zinapatana ya kwamba nchi zote zinaweza kupeleleza anga za nje lakini hakuna haki ya nchi yeyote juu yake. Inakataliwa upeleka silaha za nyuklia angani.

Mkata uliofuata wa 1979 juu ya mwezi unadai ya kwamba mamlaka juu ya magimba yote ya angani yawe mkononi wa jumuiya ya kimataifa. Lakini hadi sasa nchi zilizopeleka wanaanga nje ya angahewa hakuitilia sahihi.

Viungo vya Nje

hariri
  Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Anga-nje kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.