Annie Payep
Annie Payep (alizaliwa tarehe 28 Oktoba, 1984) ni mwandishi wa habari kutoka Kamerun, mtayarishaji wa televisheni, na mjasiriamali. Alifanya kazi kama mtangazaji wa televisheni katika kituo cha pan-Afrika VoxAfrica kuanzia mwaka wa 2009 hadi 2019 na aliteuliwa kuwa Naibu Mkurugenzi Mkuu anayehusika na ofisi ya Douala mnamo mwaka wa 2015. Mnamo mwaka 2020, alianzisha kituo cha televisheni cha mtandaoni alichokipa jina la Télé Asu.
Wasifu
haririElimu
haririAnnie Payep-Nlepe alizaliwa tarehe 28 Oktoba 1984, huko Douala. Alisoma katika chuo cha Institut Siantou huko Yaoundé, ambapo alipata Cheti cha shahada ya Juu (BTS) katika Uandishi wa Habari mnamo mwaka wa 2005. Pia anashikilia Shahada ya Sayansi na Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (DSSTIC) yenye utaalamu katika uandishi wa habari kutoka katika Ecole Supérieure des Sciences et Techniques de l'Information et de la Communication huko Yaoundé
Marejeo
haririMakala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Annie Payep kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |