Antelmi wa Belley, O.Cart. (Chignin, Chambery, Ufaransa, 1107 - Belley, Ufaransa, 26 Juni 1178) alikuwa askofu wa mji huo kuanzia mwaka 1163 hadi kifo kifo chake[1].

Alivyochorwa.

Baada ya kuingia ukleri, alipofika umri wa miaka 30 aliingia katika monasteri ya Wakartusi huko Chartreux akaijenga upya baada ya theluji nyingi kuibomoa.

Miaka 2 baadaye akawa priori bora kwa miaka 22, isipokuwa katikati alikwenda kuishi upwekeni kwa miaka michache.

Katika wadhifa huo aliitisha mkutano mkuu wa mapriori wote 8 akawa mkuu wa kwanza wa shirika lote la Mt. Bruno.

Alijitahidi kwa imara isiyochoka kurekebisha maadili ya wakleri na masharifu wa jimbo lake.

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 26 Juni[2].

Tazama pia hariri

Tanbihi hariri

Marejeo hariri

  • Attwater, Donald and Catherine Rachel John. The Penguin Dictionary of Saints. 3rd edition. New York: Penguin Books, 1993. ISBN 0-14-051312-4.

Viungo vya nje hariri

 
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.