Antioko IV wa Syria alijiita Epifane (kwa Kigiriki Ἀντίοχος Ἐπιφανής) akitaka kujitambulisha kama tokeo la mungu mmojawapo. Lakini watu walimuita Epimane, yaani kichaa, kutokana na madai yake yasiyo na kiasi.

Sanamu ya Antioko IV kwenye Altes Museum huko Berlin (Ujerumani).

Aliishi miaka 215 KK164 KK akitawala dola la Waseleuki kuanzia mwaka 175 KK hadi kifo chake.

Juhudi zake za kueneza ustaarabu wa Ugiriki wa kale kati ya Wayahudi zilishindwa na Wamakabayo waliopigania uhuru wa dini kama inavyosimuliwa katika kitabu cha kwanza cha Wamakabayo na kitabu cha pili cha Wamakabayo (ambavyo ni kati ya Deuterokanoni).


Mina ya Antioko IV Epifane.

Viungo vya nje hariri