Ugiriki ya Kale

(Elekezwa kutoka Ugiriki wa kale)

Ugiriki ya Kale ni kipindi cha historia ambapo Ugiriki ulipanuka katika eneo kubwa la Mediteraneo na Bahari Nyeusi, na kudumu kwa karibu milenia moja, hadi Ukristo ulipoanza. Wakati wa Yesu, kitovu cha ustaarabu huo kilikuwa mji wa Aleksandria (Misri).

Athena,Ugiriki

Unadhaniwa na wanahistoria wengi kuwa ni utamaduni anzilishi wa ustaarabu wa magharibi lakini iliathiri pia elimu ya Waislamu.

Wanafalsafa na wataalamu wake wa fani mbalimbali waliweka misingi muhimu ya maendeleo ya sayansi katika karne zilizofuata.

Hata baada ya Ugiriki kuingizwa katika Dola la Roma, utamaduni wa Kigiriki ulikuwa na nguvu kubwa ya ushawishi.

Maendeleo ya elimu katika himaya ya Uislamu yalitegemea kwa kiasi kikubwa kazi ya ufasiri wa vitabu vya Wagiriki kwenda lugha ya Kiarabu.

Ugiriki ya kale umeathiri pia lugha, siasa, mifumo ya elimu, falsafa, sayansi, sanaa, ufundi sanifu wa Dunia ya kisasa, na kuchochea Mwamko Mpya katika Ulaya Magharibi; na kuchipuka tena katika vipindi mbalimbali vya uamsho wa tamaduni za kisasa za Kigiriki, ndani ya karne ya 18 na ya 19 katika Ulaya na Amerika.

Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Ugiriki ya Kale kama enzi zake au matokeo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.