Arkadi, Paskasi na wenzao

Arkadi, Paskasi na wenzao Probo, Eutikiani na Paulilo (karibu wote walifariki Afrika Kaskazini, 437) ni kati ya waumini wa Kanisa Katoliki walioteswa kikatili sana na Wavandali katika karne ya 5, wakati wa utawala wa mfalme Genseriki aliyekuwa Mwario.

Wazaliwa wa Hispania, walikuwa askari wa mfalme huyo, Paskasi na Eutikiani walikuwa ndugu na Paulilo alikuwa mdogo wao.

Walipokataa kujiunga na Uario, walifilisishwa, walipelekwa uhamishoni, waliteswa na hatimaye kuuawa, isipokuwa mtoto Paulilo alifanywa mtumwa.

Tangu kale wanaheshimiwa kama watakatifu wafiadini.

Sikukuu yao huadhimishwa tarehe 13 Novemba.

Tazama piaEdit

TanbihiEdit

  Makala hii kuhusu Mkristo huyu bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Arkadi, Paskasi na wenzao kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.