Asphalt 8: Airborne

Asphalt 8: Airborne ni mchezo wa video wa 2013, uliotengenezwa na Gameloft Barcelona na kuchapishwa na Gameloft kama sehemu ya mfululizo wa Asphalt unaoendelea.

Nembo ya Asphalt 8: Airborne.

Iliachiliwa mnamo 22 Agosti, 2013 kwa iOS na Android, 13 Novemba kwa Windows 8, 15 Januari, 2014 kwa BlackBerry 10. na 5 Aprili, 2015 kwa Tizen. Muendelezo wa mchezo huu yaani mrithi utakuwa ni Asphalt 9: Hadithi ilitangazwa mnamo tarehe 26 Februari, 2018. Mchezo huo una wachezaji wapatao milioni 350, kulingana na maelezo Google playstore na Microsoft store.

Maeneo

hariri

Asphalt 8: Airborne lilikuwa na maeneo tisa tofauti wakati linatolewa, maeneo mengine zaidi ya tisa yameongezwa kupitia visasisho(updates). Maeneo yanayopatikana hivi sasa ni Nevada, Iceland, Tokyo, Guiana ya Ufaransa, London, Barcelona, Alps, Venice na Monaco (sasa Azure Coast inaongezwa hivi karibuni).

Mchezo wa wengi (Multiplayer)

hariri

Katika mchezo huu wachezaji wanaweza kucheza wawili hadi wanne wakiwa karibu mahali popote kupitia Wi-Fi, na kimataifa kupitia mtandao. Mfumo huu wa Multiplayer uliundwa mnamo Oktoba 2016, Watu wengi hushindana mtandaoni ili kushinda tuzo mbalimbali za kipekee.

  Makala hii kuhusu mambo ya michezo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu zaidi kuhusu Asphalt 8: Airborne kama historia yake, uenezi au kanuni zake?
Labda unaona katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine habari zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.