Android ni jina la aina ya mfumo huria wa uendeshaji wa simu za mikononi. Mfumo huo hutumiwa hasa katika simujanja, kama vile Google inavyomiliki Google Nexus, vilevile kampuni nyingine zinafanya vivyohivyo ikiwa ni pamoja na HTC na Samsung. Mfumo huo wa uendeshaji umepata kutumika pia katika kompyuta bapa kama vile Motorola, Xoom na Amazon Kindle Fire. [1]

Google imetoa pia Android nyingine kama vile Android TV ya televisheni, Android Auto ya magari, Android Things kwa ajili ya vifaajanja na Wear Os ya saa ya mkononi. Aina nyingine za Android hutumiwa pia kwa michezo ya kompyuta na kamera za kidijiti.

Android mwanzoni iliundwa na Android Inc. kabla ya kununuliwa na Google mwaka 2005. Matumizi rasmi ya kibiashara yalianza mnamo Septemba 2008. Toka mwaka huo Android imetoa matoleo mbalimbali. Toleo la sasa ni 9 "Pie" lililotolewa Agosti 2018. Android Q beta ilitolewa Machi 13, 2019. Programu ya msingi ya Android inaitwa Android Open Source Project (AOSP) ambayo hutolewa kwa Leseni ya Apache.

Google inasema zaidi ya simujanja milioni 1.3 zenye mfumo wa Android zinauzwa kila siku.[2] Hii imeifanya Android kuwa miongoni mwa mifumo ya uendeshaji wa simu inayotumika sana duniani.

Programu za Android

hariri

Programu za Android, zinaitwa "apps" za simu za mkononi, ambazo zinatoka duka la Google Play. Programu hizi zinatumia mtindo wa .apk. Programu za Android zimetengenezwa na lugha ya Python, C, C++, au lugha za Java lakini Kusano za mtumiaji daima hutengenezwa kwa kutumia Java na XML. Kuna apps zaidi ya milioni 2.8 zinapatikana katika Android.[3]

Kati ya programu hizi kuna apps za manufaa kama vile za kusaidia utendaji kazi wa simu kwa mfano app ya kusaidia utendaji kazi wa simu mtu akicheza michezo ya simu[4], burudani kama vile muziki na michezo ya simu na apps za kulaghai watumiaji au za kutumia kufanya ulaghai kama vile apps za kufichua nenosiri au kuiba mtandao wa intaneti. Ni muhimu mtu kuwa na uhakika na apps anazoziweka kwa simu yake.

Matoleo ya Android na majina yake

hariri
Samsung Galaxy yenye toleo la Android

Kila toleo la bidhaa la Android lina namba na jina linatokana na majina ya vitu vitamutamu. Namba za matoleo na majina yake ni:

  • Matoleo ya Beta: Ni Astro na Bender
  • 1.5: Cupcake
  • 1.6: Donut
  • 2.0 and 2.1: Eclair
  • 2.2: Froyo (Frozen Yogurt)
  • 2.3: Gingerbread
  • 3.x: Honeycomb (a tablet-only version)
  • 4.0: Ice Cream Sandwich
  • 4.1, 4.2 and 4.3: Jelly Bean
  • 4.4: KitKat
  • 5.0 and 5.1: Lollipop
  • 6.0 and 6.0.1: Marshmallow[5]
  • 7.0 and 7.1: Nougat
  • 8.0 and 8.1: Oreo [6]
  • 9.0: Pie
  • 10
  • 11
  • 12
  • 13
  • 14
Jina la
Toleo
Nambali ya
Toleo
Linux Kernel
inayotumika
Tarehe ya
Uzinduzi
kiwango cha
API
(Haina Jina la Toleo) 1.0 dunno 2008 Septemba 23 1
Petit Four (jina lisilo rasmi) 1.1 2.6.X 2009 Februali 9 2
Cupcake 1.5 2.6.27 2009 Aprili 27 3
Donut 1.6 2.6.29 2009 Septemba 15 4
Eclair 2.0 – 2.1 2.6.29 2009 Oktoba 26 5 – 7
Froyo 2.2 – 2.2.3 2.6.32 2010 Mei 20 8
Gingerbread 2.3 – 2.3.7 2.6.35 2010 Decemba 6 9 – 10
Honeycomb 3.0 – 3.2.6 2.6.36 2011 Februari 22 11 – 13
Ice Cream Sandwich 4.0 – 4.0.4 3.0.1 2011 Oktoba 18 14 – 15
Jelly Bean 4.1 – 4.3.1 3.0.31 to 3.4.39 2012 Julai 9 16 – 18
KitKat 4.4 – 4.4.4 3.10 2013 Oktoba 31 19 – 20
Lollipop 5.0 – 5.1.1 3.16.1 2014 Novemba 12 21 – 22
Marshmallow 6.0 – 6.0.1 3.18.10 2015 Agosti 5 23
Nougat 7.0 – 7.1.2 4.4.1 2016 Agosti 22 24 – 25
Oreo 8.0 – 8.1 4.10 2017 Agosti 21 26 – 27
Pie 9.0 4.4.107, 4.9.84, and 4.14.42 2018 Agosti 6 28
  • Coloring Boook For Kids for Android [7]

Kileta bahati

hariri
 
Kileta bahati cha Android kwenye ofisi za Googleplex mwaka 2008

Kileta bahati cha Android ni cha rangi ya kijani. Ingawa hakina jina maalum, inaaminika kuwa wafanyakazi wa Android hukiita "Bugdroid".[8]

Kilibuniwa na aliyekuwa mbunifu wa Google Irina Blok Novemba 5, 2007.

Tazama pia

hariri

Marejeo

hariri
  1. Android Project Home
  2. "There Are Now 1.3 Million Android Device Activations Per Day". TechCrunch. 2012-09-05.
  3. "Number of apps on Android Devices".
  4. Anon. "Game Booster: 2X Speed for games Android Free". Androidhackers Net (kwa American English). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2018-08-10. Iliwekwa mnamo 2018-08-13.
  5. "Introducing new Android OS Marshmallow 6.0". Android Official. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-06-09. Iliwekwa mnamo 1 June 201. {{cite web}}: Check date values in: |accessdate= (help)
  6. "Top Oreo Features". {{cite web}}: Cite has empty unknown parameters: |1= na |2= (help)
  7. Anon. "Coloring Book for Kids". Android Studio (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2018-09-13.
  8. "Archived copy". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo Januari 1, 2018. Iliwekwa mnamo Desemba 31, 2017. {{cite web}}: Unknown parameter |deadurl= ignored (|url-status= suggested) (help)CS1 maint: archived copy as title (link)

Viungo vya nje

hariri