Bahari ya Timor
Bahari ya Timor (kwa Kiingereza: Timor Sea, kwa Kiindonesia: Laut Timor; kwa Kireno: Mar de Timor) ni bahari ya pembeni ya Bahari Hindi iliyopo baina ya kisiwa cha Timor na Australia. Eneo lake ni km2 61,500 na kimo chake hufikia hadi mita 3300 lakini wastani ni mita 406 pekee.
Eneo lake linapitiwa na mfereji wa Timor. Mkondo wa Indonesia unapita hapa ulio muhimu kwa sababu unabeba maji ya vuguvugu kutoka Pasifiki kwenda Bahari Hindi.
Kuna idadi ya visiwa na miamba matumbawe yasiyo na watu pamoja na vyanzo muhimu vya kabohidrati.
Tanbihi
haririViungo vya Nje
haririWikimedia Commons ina media kuhusu: