Bendera ya Ethiopia
Bendera ya Ethiopia mara nyingi inatajwa kuwa bendera ya kwanza ya kiafrika. Rangi zake ni kijani kibichi, njano na nyekundu. Kutokana na sifa za Ethiopia za kuwa nchi ya pekee katika Afrika iliyojitetea dhidi ya uvamizi wa ukoloni. Rangi zake zilikuwa kama alama ya umoja na uhuru wa Afrika zikatumika kama rangi za Umoja wa Afrika katika bendera za nchi nyingi za Kiafrika.
Bendera ya rangi tatu ilitumika Ethiopia tangu karne ya 19 BK. Wakati wa serikali ya kifalme ilikuwa na nembo ya simba ya Yuda. Serikali ya mapinduzi ya DERG ilifuta simba na kubadilishabadilisha nembo za katikati. Tangu 1996 bendera imekuwa na nyota ya pembetatu.
Kama sifa hiyo ya kuwa bendera ya kwanza ya kiafrika ni kweli inategemea na namna ya kuangalia Afrika. Kwenye Afrika ya kijiografia jinsi inavyotajwa leo dola za Afrika ya Kaskazini ziliwahi bila shaka kutumia bendera tangu karne nyingi yaani muda mrefu kabla ya karne ya 19.
Nchi za Afrika zinazotumia rangi tatu za Ethiopia ndani ya bendera zao
haririNchi zenye bendera ya milia mlalo (kuanzia mlia wa juu)
haririNchi zenye bendera ya milia ya wima (kuanzia mlia wa kushoto)
hariri- Guinea: nyekundu-njano-kijani
- Kamerun: kijani-nyekundu-njano
- Mali: kijani-njano-nyekundu
- Senegal: kijani-njano-nyekundu Big Cartoon Database entry
Mpangilio tofauti za rangi tatu za Ethiopia
hariri- Jamhuri ya Kongo: milia tatu ya ulalo kijani-njano-nyekundu
- Benin: theluthi ya kushoto: kijani, halafu milia mbili za kulala njano-nyekundu
- Guinea Bisau: theluthi ya kushoto:nyekundu, halafu milia mbili za kulala njano-kijani
- Togo: pembe ya juu-kushoto ina mraba nyekundu, halafu milia minne ya kulala ya kijani na njano kwa kubadilishana
Bendera za kiafrika zinazotumia rangi tatu za Ethiopia pamoja na rangi mbalimbali
hariri- Jamhuri ya Afrika ya Kati
- Komori
- Mauriti
- Sao Tome na Principe
- Shelisheli
- Zambia
- Zimbabwe Big Cartoon Database entry